
MABINGWA wa soka Tanzania Bara
mwaka 1988 Coastal Union “Wagosi wa Kaya”inatarajia kucheza mechi ya
kirafiki na timu ya Mwadui ya Shinyanga
ikiwa ni sehemu ya maandalizi kwa timu zote kujiandaa na michuano wanayokabiliana nayo.
Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa
Jumatano ya wiki hii kwenye uwanja wa CCM
Mkwakwani lengo likiwa ni kukipa makali kikosi cha Coastal Union
kujiwida na mechi yao ya Ligi kuu Tanzania bara
dhidi ya Tanzania Prison itakayochezwa kwenye
uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
Akizungumza leo,Ofisa Habari wa
Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa mechi hiyo ni miongoni mwa
michezo mbalimbali ya kirafiki wanayocheza
ili kuweza kukiimarisha kikosi hicho ambacho msimu huu kimepania kufanya makubwa kwenye michuano ya Ligi kuu soka Tanzania.
Hata hiyo aliwataka wadau wa soka
mkoani hapa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo ikiwemo
kuangalia wachezaji ambao wamesajiliwa msimu huu kwa ajili ya michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara.
Hata hivyo alisema kuwa baada ya
kumalizika mechi hiyo wataangalia
uwezekano wa kucheza mechi nyengine ya kirafiki kabla ya kutua jijini
Mbeya ambapo watakwenda kucheza mechi yao ya Ligi kuu.
uwezekano wa kucheza mechi nyengine ya kirafiki kabla ya kutua jijini
Mbeya ambapo watakwenda kucheza mechi yao ya Ligi kuu.
No comments:
Post a Comment