WATANZANIA
wameombwa
kuvisaidia vituo vya kulelea watoto na vijana wenye ulemavu katika jamii ili
kuzitatua changamoto mbalimbali zinazowakabili hususan umaskini uliokithiri kwa
wazazi ambao ni wanawake waliotelekezwa na waume zao.
Hayo ameyasema mratibu wa kituo cha
kuwalelea watoto na vijana wenye ulemavu katika jamii (Y D C P) kilichopo
jijini TANGA William Henry wakati akitoa ufafanuzi wa changamoto
inayowakabili kituoni hapo kwa wadau wakiwemo viongozi wa serikali na sekta
mbalimbali katika semina ya siku mbili iliyofanyika kwa lengo la kuwapa
viongozi hao uelewa juu ya changamoto inayowakabili.
Aidha amesema kutokana changamoto nyingi
zinazowakabili ni vyema jamii ya watanzani iwaunge mkono ili kuweza kuwa jaili
na kuwatunza watu wenye ulemavu pamoja na watoto kwa mchango wao wa hali na
mali.
Hata hivyo
Henry ametaja changamo zinazowakabili kuwa ni pamoja na shule kwa ajili ya
elimu jumuishi.
Kwa upande Naibu meya wa jiji la Tanga Mzamini
Shemdoe amewataka viongozi wote pamoja na madiwani waliohudhuria saemina hiyo
wazingatie mafunzo hayo ambayo wameyapata na kuchukua hatua ili kujibu
changamoto ambayo wameelezwa na kituo hicho.

No comments:
Post a Comment