HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Saturday, 20 December 2014

BURUDANI:BOBAN AKANA KULIPWA MSHAHARA NA DIAMOND, HATIMAYE AISHA MADINDA AZIKWA..!!


BOBAN AKANA KULIPWA MSHAHARA NA DIAMOND PLUTNUMZZ
Maestro midfield wa zamani wa Simba SC, Haruna Moshi ‘Boban’, amekanusha vikali taarifa zilizoibuka hivi karibuni za kulipwa mshahara na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ baada ya kutua kwenye timu ya Friends Rangers inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.
Hivi karibuni, vyombo mbalimbali vya habari viliripoti taarifa za msanii huyo kujitolea kumlipa mashahara kiungo mshambuliaji huyo aliyetesa akiwa Simba Sh 400,000 kwa mwezi.
Boban alisema kuwa anashangaa kusikia taarifa hizo na hajui zimetokea wapi na kuwataka watu kujua kwamba hazina ukweli hata kidogo.

BAADA YA POLISI KUUSHIKILIA MWILI WA AISHA MADINDA HATIMAYE AZIKWA. MNENGUAJI wa zamani wa bendi ya Twanga Pepeta, Aisha Mbegu maarufu Aisha Madinda amezikwa jana katika makaburi ya Kibada, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Madinda aliyefariki dunia ghafla Jumatano wiki hii, alizikwa jana baada ya kuwa Polisi imetoa mwili wake baada ya juzi kuzuia maziko yake ili kwanza kufanyia uchunguzi mwili huo kutokana na kifo hicho kisicho cha kawaida cha mnenguaji huyo aliyejipatia umaarufu mkubwa nchini.

Msanii huyo ambaye katika siku za mwisho alijiunga na bendi ya Extra Bongo chini ya uongozi wa Ali Choki, kifo chake kinaaminika kuwa kimesababishwa na matumizi ya dawa za kulevya, na siku ya kifo chake, alikutwa hajitambui akiwa barazani kwenye nyumba ya rafiki yake aliyetambuliwa kwa jina la Samira Saleh, eneo la Mabibo katika Manispaa ya Kinondoni.
Choki pamoja na aliyewahi kuwa bosi wake, Asha Baraka mmiliki wa Twanga Pepeta, walikuwa miongoni mwa maelfu ya waombolezaji walioshiriki maziko hayo kuanzia mwili wake ulipowasili nyumbani kwao Mikwambe, Kigamboni.

No comments:

Post a Comment