Waandishi: Rebeca Duwe Na Daniel Shemjawa ,TANGA.
Kutokana na kasi ya ongezeko la
makanisa hapa nchini baadhi ya Wachungaji wa makanisa mbalimbali jijini Tanga
wameeleza wasawasi wao na kusema kuwa utitiri wa madhehebu kwa sasa sio mpango
wa Mungu bali upotevu wa utimilifu wa imani.
Wakizungamza na Mtandao huu kwa nyakati
tofauti wachungaji hao walikuwa na haya ya kusema
Mch.kiongozi wa kanisa
la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Mlingano wilayani
Muheza mkoani Tanga Mch.Samweli Mteri alisema kasi ya ongezeko la
madhehebu ya makanisa mbalimbali imeonekana kuwa sio mpango wa Mungu bali ni
nguvu za shetani .
Aidha alisema watumishi wanapaswa
kuatambua nyakati na majira na kuacha tamaa ya fedha na badala yake wamtumikie
Mungu kama neno lilivyosema hubirini injiili ulimwenguni mwote na kwa
kilia kiumbe na wala sio kwa ajili ya maslahii yao binafsi.
Hata hivyo alisema wakristo waache tabia ya kuhangaika kwa kutafuta miujiza kwa watu nguvu za giza huku wqakitaja jina la yesu na badala yake waamue wenyewe kumwomba Mungu ili awajibu mahitaji yao.
Hata hivyo alisema wakristo waache tabia ya kuhangaika kwa kutafuta miujiza kwa watu nguvu za giza huku wqakitaja jina la yesu na badala yake waamue wenyewe kumwomba Mungu ili awajibu mahitaji yao.

Kwa uapande wake Mch..Ernest
Kangajaka wa Kanisa la Jerusalem Spiritual Transformation Church (J S T C)
lililopo jijini Tanga aliwataka wakristo kuchukua tahadhari na kuacha tabia ya
kuhamahama makanisa na badala yake watulie mbele za Mungu wao na kutafuta uso
wa Mungu kwani Mungu humsikliza mtu yule ambaye anaomba katika kweli bila ya
wasiwasi.
Kangajaka yeye alieleza msimamo wake kuhusu kasi ya kuongezeka kwa makanisa kuwa makanisa yaendelee kuongezeka ila tupime roho zile ambao zinafanya kazi ndani hayo makanisa kwani manabii wameongezeka kwa kasi kubwa katika ulimwengu wa sasa kama ambavyo Yesu alivyotabiri kuwa nyakati za mwisho kutakuwa na manabii wa uongo na wapinga kristo.

Hata hivyo alisema Waanzilishi wa
makanisa wale ambao wanaijua msingi wa imani yao wachukue watua ya
kuwaonya wale ambao hawaendi kwa utaratibu nadani ya makanisa yao ili kusudi
jina la Mungu lisiaibike kwani kupitia baadhi ya wachunagaji au manabii
waliojitokeza, jina la Mungu limetukanwa kwa matendo maovu yaliyofanyika
kupitia huduma yao.
Alitolea mfano wa watu wanaomwabudu
Mungu wa Eliya kuwa ni uongo kwani Mungu ni mmoja tu aliyeumba mbingu na nchi
hivyo ni jukumu la klia mkristo kutambua ni roho gani inayomwongoza ili
asipotee kwa injli ya uongo bali atafute ni wapi roho yake itapona .
Naye Mch.Ishmael Ngoda wa kanisa la
kilutheri la kiinjili Tnazania (KKKT) Usharika wa Kisosora jijini Tanga alisema
kuna haja kubwa ya wakristo kutambua nyakati tulionayo ni aina gani hivyo
kutokana na kasi ya ongezeko la madhehebu ni jukumu letu sote kutambua kuwa
tunaelekea wapi au tunaenda wapi "alisema".
No comments:
Post a Comment