Na Rebeca Duwe.TANGA
WIZARA ya afya na Ustawi
wa Jamii imetoa tunzo ya BIMOC kwa Kituo cha afya cha Pongwe pamoja na vyeti
maalum vya daraja la kwanza.
Hatua
hii imekuja baada ya kuridhika na huduma
bora ya dharura kwa wanawake wajawazito
na watoto inayotolewa na kituo hicho.
Akifafanua
maana ya BIMOC katika hafla fupi iliyofanyika kituoni hapo hii leo mganga mkuu
Faisal Ally, mara baada ya kupokea tunzo hiyo amesema hiyo ni kuonyesha kuwa
kituo hicho ni bora kwa huduma ya mama na mtoto
Sanjari
na hayo pia Mganga huyo ameelezea uwezo mwingine walionao kituoni hapo kama
vile kufanya upasuaji, kutoa dawa za usingizi, huduma ya kutoa na kuhifadhi
damu salama ambayo wanategemea kuianza hivi karibuni baada ya kukamilika kwa
mahitaji ya vifaa kadhaa.
Hata
hivyo changamoto inayowakumba katika kutoa huduma kwa mama wajawazito ambayo
hutolowa bure ameelezea kuwa ni urejeshaji wa matumizi wanayotumia kuwahudumia.
No comments:
Post a Comment