MHOLANZI
Hans van der Pluijm amewasili Saa 8:30 usiku wa kuamkia leo kwa ndege ya
Shirika la Ethiopia tayari kurudi kazini Yanga SC.
Baada
ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es
Salaam, Pluijm alisema amefurahi kurudi Yanga SC na hiyo inamaanisha ndoto zake
zimetimia.
“Nimefanya
mazungumzo na Yanga, natarajia nitasaini Mkataba baadaye (leo), sasa nakwenda
kupumzika kwanza,”alisema.
Imefahamika
kuwa kocha msaidizi Mkwasa alishasaini tayari mkataba wa kuifundisha Yanga wiki
iliyopita!

No comments:
Post a Comment