Mwalimu wa shule ya
umma nchini Uingereza amepatikana na hatia ya kuwalawiti watoto wanaorandaranda
mitaani nchini Kenya.Simon Harris alipatikana na hatia ya makosa saba, ikiwemo
kuwadhulumu kingono watoto hao katika mji wa Gilgil.
Alipatikana
na hatia katika mahakama ya Birmingham kwa makosa manne ya kumiliki picha chafu
zinazoonyesha uchi wa waoto wadogo.
![]() |
| Simon Harris |
Hata
hivyo mahakama haikumpata na hatia ya kitendo cha kuwabaka watoto hao.Haris
alikuwa anakabiliwa na maskosa 23 ikiwemo madai 18 ya kuwadhulumu watoto.
Unyama
huo ulitendwa wakati Harris alipokuwa anaendesha shirika la kijamii la
kuwasaidia watu mapema mwaka wa 1990.Wakati kesi yake ilipokua inaendelea,
wendesha mashitaka walisema kuwa aliwahadaa watoto hao wavulana kwenda nye
nyumbani kwake iliyojulikana kama "The Green House", kwa kuwapa
chakula na kuwapa hifadhi.
Kabla
ya kesi hio kuanza, Harris alikiri makosa sita ya kuwadhuru watoto hao waliokuwa
kati ya umri wa miaka 13-14 alipokuwa bado mwalimu wa chuo cha Davon.
Awali
alikuwa anakabiliwa na makosa 22 kuhusiana na dhuluma hizo alizozitenda nchini
Kenya lakini jaji Philip Parker QC alisema kuwa makosa manne dhidi ya mtuhumiwa
yaliodnolewa wakati kesi hio ilipokuwa inasikilizwa.

No comments:
Post a Comment