HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Wednesday, 17 December 2014

"TANZIA" MNENGUAJI AISHA MADINDA AFARIKI DUNIA..!!


Aisha Madinda enzi za Uhai Wake

Aliyekuwa Mnenguaji na Muimbaji wa Bendi ya Twanga Pepeta Aisha Madinda amefariki dunia hivi punde Jijini Dar es salaam. 

Habari imethibitishwa na mmiliki wa bendi ya Twanga pepeta Asha Baraka. 

Mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta amesema kuwa alipewa taarifa na Daktari mmoja kuwa wameona kama mwili wa Aisha Madinda hospitalini hapo, ndipo akatuma watu kwenda kuangalia akiwemo Luiza Mbutu ili kuhakikisha kama kweli ni yeye ndipo walipogundua ni yeye.

“ Mimi nipo njiani natoka Kigoma kuja Dar es Salaam, ni habari ya kusikitisha sana maana Aisha amefariki katika mazingira ya kutatanisha sana, jana alikuwa mzima na anachati na watu kwenye simu leo napigiwa simu mwili wake umekutwa umehifadhiwa kwenye hospitali ya Mwananyamala, hata sielewi nini kimetokea”. Amesema Asha Baraka

Mungu ailaze roho ya Marehemu Aisha Madinda mahali pema peponi , Amina "Kwa hisani ya http://www.jamiiforums.com

No comments:

Post a Comment