Dodoma. Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imetangaza matokeo ya awali ya uchaguzi wa
Serikali za mitaa nchi nzima yanayoonyesha kuimarika kwa upinzani.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Tamisemi), Khalist Luanda alisema jana kwamba
wakati CCM ikifanikiwa kupata ushindi wa jumla mitaa na vijiji 9,406, kwa
pamoja vyama vingine vya upinzani, vimegawana nafasi 3,211.
Kwa
ushindi huo upinzani umeongeza viti 1,981 ikilinganishwa na uchaguzi wa
Serikali za Mitaa uliopita mwaka 2009 ambao kwa ujumla, ulipata nafasi 1,230 za
wenyeviti wa mitaa na vijiji.Kwa upande wake, CCM imepoteza nafasi 2,636 za
uenyekiti wa vijiji na mitaa ikilinganishwa na uchaguzi wa mwaka 2009 ilipopata
jumla ya viti 12,042.
Hata
hivyo, uchaguzi mwa mwaka huu, umefanyika huku kukiwa na nyongeza ya mikoa,
wilaya, mitaa na vijiji katika baadhi ya maeneo nchini.
Luanda
alisema CCM kimepata vijiji 7,290 kikifuatiwa na Chadema yenye vijiji 1,248.
CUF imeshika nafasi ya tatu kwa kuwa na vijiji 946, ikifuatiwa na UDP yenye
vinne na TLP na NLD vyenye viwili kila kimoja.Katika nafasi za wenyeviti wa
mtaa, CCM kimechukua jumla ya mitaa 2,116. Vyama vingine na nafasi zao kwenye
mabano ni Chadema (753), CUF (235), ACT (9), NCCR - Mageuzi (8) wakati vyama
vya TLP, UMD, UDP na NRA vimepata mtaa mmoja kila kimoja.
![]() |
| VIONGOZI WA UKAWA |
Matokeo
hayo yamejumuisha maeneo mengi ambayo CCM ilipita bila ya kupingwa.Katika
matokeo hayo, CCM imeendelea kufanya vizuri katika mikoa ambayo imekuwa
ikitajwa kuwa ni ngome yake lakini kuna maeneo ambayo yalionekana kuyumba kwa
kuzolewa na upinzani.
Mfano wa
ngome ambazo CCM kimetikiswa zaidi ni Mkoa wa Dodoma katika wilaya za Kondoa na
Chemba ambako vyama vya CUF na Chadema vimefanya vizuri tofauti na uchaguzi
uliopita.Kuhusu nafasi ya mwenyekiti ambaye alisimikwa na wananchi kibabe
katika Mkoa wa Arusha, Luanda alisema Tamisemi haitamtambua, bali atakuwa ni
mwenyekiti wa kimila tu.
CHANZO:TOVUTI YA MWANANCHI

No comments:
Post a Comment