Shirikisho
la Soka la Kimataifa (Fifa) limeiagiza Etoile du Sahel kulipa kitita cha dola
300,000 (Sh milioni 480) pamoja na faini.
Fifa imeitaka klabu hiyo ya Sousse nchini Tunisia
kuhakikisha inalipa fedha hizo ndani ya mwezi mmoja pamoja na faini ya dola
28,000.Hatua hiyo imefikia baada ya Simba kushinda kesi iliyotokana na Simba
kushitaki kwa Fifa baada ya Etoile kushindwa kulipa fedha za malipo ya kumnunua
Emmanuel Okwi.
Okwi
aliuzwa wakati wa uongozi wa Ismail Aden Rage na Etoile ikautumia mwanya huo
kuanza kuizungusha Simba.Rage aliahidi Etoile wangelipa wakati akiwa
madarakani, kabla hajaondoka, lakini haikuwa hivyo.
Zigo
likamuangukia yeye kwa kuwa ndiye aliidhinisha Okwi kwenda Etoile hata kabla ya
Waarabu hao kulipa, kabla ya kumgeuka.Etoile walizidi kusumbua baada ya Okwi
kurejea Uganda na baadaye Yanga, hali iliyofanya Simba kukata tama.
Taarifa
zinaeleza barua ya agizo hilo, tayari imetua TFF ambayo imewasilisha kwa Rais
wa Simba, Evans Aveva kwamba anatakiwa kupokea mzigo pamoja na faini hiyo ndani
ya mwezi mmoja.Tayari Okwi ameisharejea Simba akitokea Yanga, hivyo Simba
itafaidika kuwa na mchezaji halafu na mkwanja juu.
No comments:
Post a Comment