Wakurugenzi
17 wa halmashauri nchini, wameshughulikiwa baada ya kuvurunda katika uchaguzi
wa serikali za mitaa uliofanyika Jumapili iliyopita.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),
Hawa Ghasia, jana alitangaza kutengua uteuzi wa wakurugenzi sita, kusimamisha
watano, kuwapa onyo kali watatu na kuwapa onyo wakurugenzi watatu.
Hata
hivyo, licha ya makundi kadhaa ya jamii kumtaka Ghasia awajibike sambamba na
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutokana na uchaguzi huo kukumbwa na kasoro nyingi,
alikataa kujiuzulu.
![]() |
|
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),
Hawa
Ghasia
|
Badala
yake, alisema hatawajibika kwa kuwa ameshachukua hatua dhidi ya wakurugenzi hao
na kwamba amejipima na kuona anatosha.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam jana kutangaza maamuzi
hayo, Ghasia alisema wakurugenzi hao wamechukuliwa hatua mbalimbali na
tayari Rais ameridhia hatua hizo.
“Kutokana
na ripoti tulizopokea kuhusu masuala yaliyojitokeza katika uchaguzi huu, ni
dhahiri kuwa wakurugenzi wa halmashauri zenye dosari wameonyesha udhaifu mkubwa
katika kutekeleza jukumu la usimamizi wa uchaguzi ambalo ni moja ya majukumu ya
Ukurugenzi, ” alisema.
Alisema
wakurugenzi hao wamefanya makosa matano ambayo ni kuchelewa kuandaa vifaa vya
kupigia kura, kukosa umakini, kuchelewesha vifaa, uzembe na kutoa taarifa za
kupotosha.
“Kutokana
na udhaifu waliouonyesha wakurugenzi hao kwa mamlaka aliyonayo chini ya Ibara
ya 36 (1) (4) ya Katiba Rais ameridhia wachukuliwe hatua zifuatazo ambazo ni
kutengua uteuzi, kusimamishwa kazi, kupewa onyo kali na kupewa onyo,” alisema.
WALIOSIMAMISHWA
Waziri
Ghasia aliwataja wakurugenzi waliosimamishwa kazi na halmashauri zao kwenye
mabano kuwa ni Felix Mabula (Hanang’), Fortunatus Fwema (Mbulu), Isabela
Chilumba (Kwimba) na William Shimwela (Manispaa ya Sumbawanga).
Alisema
waliosimamishwa kazi ya ukurugenzi, watapisha uchunguzi zaidi wa kiwango cha
ushiriki wao katika kasoro zilizojitokeza kwenye halmashauri zao.
WALIOTENGULIWA
UTEUZI
Alisema
wakurugenzi ambao uteuzi wao umetenguliwa ni Benjamin Majoya (Mkuranga),
Abdallah Ngodu (Kaliua), Masalu Mayaya (Kasulu), Goody Pamba (Serengeti),
Julius Madiga (Sengerema) na Simon Mayeye (Bunda).
Alisema
waliotenguliwa uteuzi watapangiwa kazi za taaluma zao wakati uchunguzi zaidi ukiendelea
ili kubaini dhamira ya vitendo vyao.
WALIOPEWA
ONYO KALI
Katika
mtikisiko huo, wakurugenzi watatu wamepewa onyo kali ambao ni Mohamed Maje
(Rombo), Hamis Yuna (Busega) na Jovin Jungu (Muheza).
Kwa
mujibu wa Ghasia, waliopewa onyo kali, pia watawekwa chini ya uangalizi kubaini
kama wana udhaifu mwingine ili wachukuliwe hatua zaidi.
WALIOPEWA
ONYO
Aidha,
wakurugenzi wengine watatu wamepewa onyo ambao ni Isaya Mngulumi (Ilala),
Melchizedeck Humbe (Hai) na Wallace Karia (Mvomero).
Waliopewa onyo alisema
wanatakiwa kuongeza umakini wanapotekeleza majukumu yao.Waziri Ghasia alisema:
“Nimechukua hatua na Rais ameridhia. Mimi

No comments:
Post a Comment