Aliyekuwa Kocha wa Kiungo mkenya Victor Wanyama
anaechezea klabu ya Southampton ya Uingereza James Nandwa ameingia mkataba wa
mwaka mmoja na vogogo wa Soka mkoani Tanga COASTAL UNION.
![]() |
| James Nandwa kulia |
Kocha huyo anachukua mikoba iliyoachwa na Kocha
Yusuph Chippo aliyekwenda nchini kwao Kenya kutokana na matatizo ya kifamilia
kuwa kwenye hali ambayo sio nzuri jambo ambalo lilipelekea kushindwa kurudi
nchini kwa ajili ya kuendelea kukinoa kikosi hicho.
Akizungumza mara baada ya kutua jijini Tanga jana na
kulakiwa na vingozi wa klabu hiyo wakiongozwa na Meneja wao, Akida Machai
katibu mkuu pamoja na wajumbe wa kamati ya utendaji, Kocha huyo amesema dhamira
yake kubwa ni kuhahakikisha anaipa mafanikio makubwa timu hiyo.
Akizungumza kleo ofisa habari wa klabu hiyo Oscar
Senga amesema kuwa ujio wa Kocha huyo utawezesha timu yao kufikia malengo
waliyo jiwekea ambayo ni kuhakikisha wanachukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania
Bara msimu huu.
Kocha Nandwaamesema kuwa kitu cha kwanza ni
kuhakikisha timu hiyo inafikia malengo yake ya kuwa timu bora Tanzania na
hatimaye ipate nafasi ya kushikiriki michuano ya kimataifa.
Kocha huyo aliwahi kuzifundisha timu za Soka za
Harambee Stars,AFC Leopard na Utalii zote za Kenya na kuzipatia mafanikio
makubwa.

No comments:
Post a Comment