Matukio ya kumatwa kwa Wahamiaji Mkoani Tanga yamezidi
kushamiri ambapo mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la Ally Mbukuzi mwenye umri wa miaka 17 mkulima na mkazi
wa Putini kata ya Chongoleani Wilaya ya Tanga kwa kosa la kuwaasafirisha
wahamiaji haramu wapatao sita (6) ambao ni Raia wa Ethiopia.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Tanga Frasser Kashai amesema kuwa mnamo tarehe 8 Disemba
mwaka huu majira ya saa saba 13:00 mchana, huko katika kisiwa cha Jambe Kata ya Tongoni Tarafa ya
Pongwe Wilaya Tanga wamekamatwa wahamiaji hao ambao wametambulika kwa majina ya
Dolec Dalalo umri wa miaka 28, Alaleus
Tesame umri wa miaka 21, Hashinavia Shamibu umri wa miaka 23, Taken
Ndasalh umri wa miaka 20,Tamesgen Kisfon umri wa miaka 20, Mihon Eriamin umri
wa miaka 22.
Aidha
mtuhumiwa amekiri kufanya kufanya biashara hiyo ya usafirishaji wa wahamiaji
haramu hivyo atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi wa awali kukamilika.
Katika tukio jingine Gari yenye namba za usajili T.131
AZZ SCANIA mali ya kampuni ya Saibaba limekamatwa likiwa na Raia 12 wa
Ethiopia likiwasafirisha kutokea Arusha kuelekea jijini Dar es salaam
Raia
hao wamekamatwa majira ya saa 10:30 jioni maeneo ya Mbwiko Kata ya Mbwiko
Tarafa ya Mombo barabara kuu ya Mombo –Segera Wilayani Korogwe.
Kamanda
kashai amewataja Raia hao kuwa ni Kashoma Bayen umri wa miaka 24,Berchano
Gamada umri wa miaka 32, Awal Jamal umri
wa miaka 23 ,Yanis Gatiso umri wa miaka 28,
Metson Sipril umri wa miaka 21,Tashona
Hayalis umri wa miaka 30.
Wengine
ni Adino Samiru umri wa miaka 20, Kengeny
Siyun umri wa miak 22 ,Charnes Egesa umri wa miaka 20, Abdi Bandru umri
wa miaka 21, Siumanda Siumanda umri wa miaka 26 na Na Malako Abuu umri wa miaka
23.
Watuhumiwa
wote wanashikiliwa na Jeshi la Polisi na watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma
inayowakabili pale upepelezi wa awali utakapo kamilika.
No comments:
Post a Comment