MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Hassan
Bakari mwenye umri wa miaka 55 amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kamba ya
katani aliyoifunga kwenye mti wa michungwa shambani kwake.
Akitoa
taarifa hiyo kwa Waandishi wa Habari Ofisini kwake jijini Tanga kamanda wa
Jeshi la polisi mkoa Tanga Frasser Kashai amesema tukio hilo limetokea mnamo
tarehe 8 desemba mwaka huu majira ya saa 12:00 mchana huko kijiji cha
Pangamlima kata ya Kwafungo ,Tarafa Mbwembwela Wilaya ya Muheza .
Adha
amesema chanzo cha mtu huyo kujinyonga hakijajulikana nab ado kinachunguzwa
ambapo hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
No comments:
Post a Comment