POGBA KUREJEA MANCHESTER.
Msimu wa usajili unakaribia
kufunguliwa mwezi wa kwanza huko Ulaya klabu nyingi za nchi hizo ziko kwenye
jitihada za kutaka kuboresha vikosi vyao.
Klabu ya Manchester City imeanza
mchakato wa kutaka kumchukua mchezaji kutoka kwenye timu ya Juventus Paul Pogba
ili achukue nafasi ya Yaya Toure anayetarajiwa kuondoka kwenye msimu ujao wa
usajili.
Paul Pogba alikuwa mchezaji wa klabu
ya Manchester United kabla ya kusajiliwa huko Italia kwenye klabu ya Juventus.
WEMA APAMBANA KUPATA MAFANIKIO.
“Mimi siwezi kuringia umaarufu
wakati najiona sina mafanikio, nitafanya kila mbinu nipate mafanikio makubwa
zaidi, niweze kuijenga heshima ya jina langu kwa mashabiki,” alisema.
Muigizaji Wema Sepetu, amesema
mawazo yake yamejikita kutafuta mbinu za kumwezesha kupata mafanikio zaidi.
Amesema dhamira yake, anataka kuwa
na mafanikio zaidi ya aliyonayo hivi sasa.
Wema aliyewahi kuwa Miss Tanzania,
amesema umaarufu kwake si muhimu kama, ilivyo kwa baadhi ya wasanii wengine
nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam,
Wema alisema anashangazwa na baadhi ya wasanii wanaothamini umaarufu kuliko
mafanikio.
“Mimi siwezi kuringia umaarufu
wakati najiona sina mafanikio, nitafanya kila mbinu nipate mafanikio makubwa
zaidi, niweze kuijenga heshima ya jina langu kwa mashabiki,” alisema.
Alisema, mawazo yake ameyaelekeza
zaidi kujua namna ya kupata fedha kwani ukifanikiwa, kila jambo huwa rahisi,”
alisema Wema.
ALY KIBA AFUNGUKA KUHUSU KOLABO.
“Kufanya ‘kolabo’ na mtu unayemtaka
ni maamuzi ya msanii mwenyewe, si kila mtu ajue kama unamshirikisha fulani.
Mkali wa muziki wa miondoko ya
kizazi kipya Ali Kiba, amesema hawezi kusema atamshirikisha msanii yupi baada
ya kuachia kibao cha ‘Mwana.’
Kibao hicho cha Mwana, kimeonekana
kufanya vyema, kukubalika katika soko la muziki nchini.
Kiba amesema lengo la kufanya hivyo
ni kutaka mambo yake yaende kimya kimya.
Akizungumza na Mwandishi Wetu, Kiba
alisema kuna siku, atamshirikisha Naseeb Abdul ‘Diamond’, kuwadhihirishia
mashabiki, hakuna bifu kati yao.
Alisema hakuna shabiki, aliyejua
kama angefanya nyimbo kwa kumshirikisha mwanamuziki maarufu, Robert Kelly.
Alisema anataka kuendelea na
utaratibu wa kufanya mambo kimya kimya, kuwashangaza mashabiki.
Alisema hataki kujisifu, ingawa
ukweli uko wazi yeye ni msanii mahiri, anataka kuendelea kudhihirisha hilo.
“Kufanya ‘kolabo’ na mtu unayemtaka
ni maamuzi ya msanii mwenyewe, si kila mtu ajue kama unamshirikisha fulani.
“Kuna siku nitamshirikisha Diamond,
lengo langu nataka kuwaonyesha watu kwamba hatuna ugomvi,” alisema Kiba.
DIAMOND ATAMBA KUIBEBA TANZANIA
“Ukweli mimi sina muda wa kufanya
starehe, ukinikuta nafanya starehe basi ujue hapo kuna fedha natarajia kupata,
nauthamini muziki wangu, sitaki niporomoke bado sijatimiza ndoto zangu,”
alisema Diamond.
Naseeb Abdul ‘Diamond’ amesema ana
kazi moja tu, kuitambulisha Tanzania kimataifa kupitia muziki, hajali
wanaomfanyia majungu.
Akizungumza na Mwandishi Wetu
Diamond, alisema muziki kwake siyo starehe, anatumia muda mwingi kufikiria na
kubuni mambo yenye manufaa kwangu na Taifa kwa ujumla.
Msanii huyo alisema dhamira yake, ni
kuona Tanzania inajulikana katika anga za kimataifa, kupitia tungo zake.
Alisema baadhi ya wasanii wamekuwa
wakiendekeza starehe zaidi bila kujali kazi matokeo, yake kushindwa kupata
mafanikio waliyoyakusudia.
“Ukweli mimi sina muda wa kufanya
starehe, ukinikuta nafanya starehe basi ujue hapo kuna fedha natarajia kupata,
nauthamini muziki wangu, sitaki niporomoke bado sijatimiza ndoto zangu,”
alisema Diamond.
Aliwataka wasanii wezake wasiwe
wachoyo, wadumishe upendo ambao utawezesha kupiga hatua kupitia tasnia ya
muziki.
No comments:
Post a Comment