
WAKAZI wa Jiji la Tanga wametakiwa
kukitumia kituo kipya cha mabasi yaendayo mikoani na wilayani kilichopo Kange
ingawa
bado kuna baadhi ya changamoto za
kukamika kwake.
Rai hiyo ilitolewa na Mstahiki Meya
wa Jiji hilo, Omary Gulledy alipozungumza na madiwani katika kikao cha baraza
kilichofanyika jijini hapa.
Alisema wakazi wa Tanga wasione
kimya katika umaliziwaji wa kituo hicho bali ni serikali inaendelea na mchakato
wa kufikisha huduma zote muhimu kwenye stendi hiyo mpya.
Sambamba na hayo Gulledy alisema
lengo hasa la kuhamishia stendi hiyo Kange ni kulikuza jiji baada ya kituo cha
mabasi kilichokuwepo kuwa kidogo.
Kwa upande wake Naibu Meya wa jiji
hilo Mzamini Shemdoe alisema kuna mipango ya muda mfupi na mrefu kwa ajili ya
kujenga vibanda vya biashara vya muda ili kukidhi mahitaji ya wasafiri na
wakazi kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment