Maandamano
ya Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Korogwe yaliyokuwa yakiishinikiza Serikali
kutimiza Serikali kutimiza ahadi yake ya kuwapatia mikopo jana yaligonga mwamba
baada ya Askari Polisi wenye mabomu ya kutoa machozi kufanikiwa kuwatawanya waandamanaji hao.
Maandamano
hayo yalianza majira ya saa tano za Asubuhi ambapo kabla ya hapo waandamanaji
waliasisi mgomo wa kutokula chakula chochote wala kuingia Darasani hadi hapo madai yao ya Msingi
yatakapo tekelezwa.
Mmoja
wa wandamanaji hao ambaye ni Kiongozi aliyeomba jina lake lihifadhiwe alisema
walifikia hatua hiyo baada ya jitihada zao za kuwasiliana na katibu mkuu Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundikugonga mwamba.
Amesema
wakati wanaomba kujiunga na chuo hicho cha alimu walielezwa kwamba wangepewa
mikopo huku wakiahidiwa kupewa upendeleo wa kusoma Diploma ya juu kwa masomo ya
Sayansi na hisabati.
Hata
hivyo wakati wakiulizia mikopo yao walipigwa mpira huku chuo cha TTC nacho
kikiwahimiza kulipa ada ya Sh 600,000/= ili kuweza kuwasajili.
Amesema
kuna baadhi yao waliweza kulipa ada hiyo huku wengine wakilipa nusu na robo ili
waweze kusajiliwa huku wakiendelea kuwasilisha kilio chao cha kutolipwa mikopo
waliyo ahidiwa na katibu Mkuu kupitia Bunge.
Ameendelea
kueleza kuwa cha kusikitisha zaidi wamekuwa wakipewa majibu ya kukatisha tamaa
wakielezwa kuwa ni siasa zilizojitokeza hivyo wao kujikuta hawana sehemu ya
kupata msaada.
“Tumepambana
tukiulizia ahadi yetu lakini tumekuwa tukipigwa mpira huku tukipewa majibu
yasiyo na tija,tulianza na mgomo wa ndani, ikaja kutokula na kuingia
madarasani na leo tunaandamana” alisema
mtoa habari huyo.
Aidha
amesema wanafunzi hao wa Ualimu wanahisi kurubuniwakatika mchakato mzima kwani
baadhai yao kama wangepewa ukweli mapema wasingeweza kujiunga na chuo hicho
kutokana na hali za familia zao kuwa duni.
Naye Mkuu wa chuo cha Ualimu Korogwe Lyana Mmbaji ameeleza
kusikitishwa kwake na maandaano hayo yasiyo rasmi ambapo amesema alilazimika
kuvipa taaraifa vyombo vya ulinzi na Usalamaili kutuliza hali ya hewa.
Mmbaji
amesema baada ya Polisi kuwatawanya waandamanaji hao mazungumzo
yaliyowakutanisha viongozi wa wanafunzi
hao wa mwaka wa kwanza nia viongozi wa Serikali Wilayani Korogwe yamekuwa
yakiendelea ambapo bado haijafahamika maazimio.
No comments:
Post a Comment