Na Godwin Henry .TANGA
ALIYEKUWA
kiungo wa Sofapaka ya Kenya, Abdulhalim Humud amesaini mkataba wa miaka miwili
kuichezea timu ya Coastal Union ya Tanga yenye maskani yake Barabara ya 11
mjini hapa.
Humud,
ambaye aliwahi kuzichezea klabu mbalimbali hapa nchini zikiwemo Simba, Mtibwa
na Azam, amehaidi kufanya makubwa kwenye kikosi cha wagosi wa kaya ambacho
kinajiwinda na michuano ya Ligi Kuu Tanzania bara.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini hapa jana, Ofisa habari wa Coastal Union, Oscar
Assenga alisema kuwa wana matumaini makubwa na mchezaji huyo ambaye alikuwa
tishio kwenye klabu alizowahi kuchezea nchini.Kwa mujibu wa Assenga, Humud
tayari ameshatua jijini Tanga na ameungana na wachezaji wenzake kwenye mazoezi
yanayoendelea kwenye viwanja wa Disuza chini ya Mkurugenzi wa benchi la ufundi
la Coastal Union, Mohamed Kampira.
Wachezaji
wengine waliosajiliwa kwenye dirisha dogo ni Bakari Sadiq kutoka Friends
Rangers ya Dar es Salaam, Godfrey Wambura ambaye alikuwa mchezaji wa Kagera
Sugar.Kwa upande wake Humud, alisema amejisikia faraja kubwa kusajiliwa na
Coastal Union na kuahidi kushirikiana na wachezaji wengine ili kuipa mafanikio
timu hiyo.
Wakati
huo huo, klabu hiyo imeingia mkataba wa mwaka mmoja na aliyekuwa kocha wa
makipa wa Yanga, Mfaume Athumani kuwanoa makipa wa kikosi hicho.
Assenga
alisema kocha huyo anachukua mikoba ya Razack Siwa aliyewahi kuwanoa makipa wa
timu hiyo kabla ya kuondoka.Assenga alisema kocha huyo aliwahi kuzifundisha
timu za soka Yanga, Ashanti United na Timu ya Taifa ya Vijana U-20, hivyo wana
matumaini makubwa ataimarisha safu ya walinda milango kwenye kikosi hicho na
kuipa mafanikio.

No comments:
Post a Comment