Polisi
nchini China wanafanya uchunguzi wa kuwasaka mabibi harusi zaidi ya mia moja
wenye asili ya Vietnam ambao walipotea katika kijiji kimoja masikini kaskazini
mwa jimbo la Hebei baada ya kuolewa .
Makuwadi waliowauza mabibi harusi kwa
wanaume wameshangazwa na kitendo cha kupotea kwa mabibi harusi pamoja na pesa
walizozipata makuwadi pia kupotea.
Wanawake hao walikuwadiwa kwa gharama ya
dola 16,000 kila mmoja.
Lakini wadadisi wa mambo wanadai kwamba
wanaume wa kichina walioko mijini wanapaswa kuwa na fedha za kutosha ili
kuwavutia wanawake wa Kichina,na hivyo imewalazimu wanaume wa kichina kununua
wanawake kutoka nje ya nchi hiyo kama Vietnam,Cambodia na Burma , zoezi
linaloonekana kushika kasi kila uchao wakilenga vijiji hohehahe.

No comments:
Post a Comment