Msichana
wa kazi aliyetikisa vyombo vya habari duniani kwa kumtesa mtoto wa miezi 18,
Arnella Kamanz aliyekuwa kwenye uangalizi wake huko Uganda, amekiri makosa
mbele ya mahaka nchini humo.
![]() |
| Tumuhiirwe |
Jolly
Tumuhiirwe, mwenye umri wa miaka 22, alifanya ukatili uliochukiwa na watu wote
Duniani, ambapo alinaswa na camera ya siri, akimtandika mtoto wa mdosi wake kwa
kumkanyaga mgongoni akiwa ameanguka chini, kumchapa na kitu kisichojulikana na
kumpiga mateke na makofi ya nguvu usoni.
Kitendo
hicho kilifuatia mtoto huyo wa kike, kushindwa kula, kutokana na kasi ya
ulishwaji ambapo Tumuhiirwe, alikuwa akimlisha mtoto huyo kwa kasi ya ajabu,
kwa kushindilia vijiko mdomoni mfululizo.
|
Rnella Kamanzi,
Binti mwenye umri wa miezi 18 tu,
aliyeteswa na Tumuhiirwe
|
Huenda
mahakama hiyo ikamuhukumu kifungo cha hadi miaka 15 jela, kulipa faini au vyote
kwa pamoja. Msichana huyo katika maelezo yake mahakamani, aliomba radhi wazazi
wa mtoto huyo, taifa la uganda na walimwengu wote waliokereka na kitendo chake
na kuomba msamaha.
Hukumu yake itatolewa Jumatano Desemba 11, 2014.
Hata
hivyo wakili wa msichana huyo wa kazi aliyekiri kosa hilo Desemba 8, 2014,
amedai kuwa mteja wake hakutendewa haki kwa vile hakuelewa mashtaka yaliyokuwa
yakimkabili.

No comments:
Post a Comment