HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Monday, 1 December 2014

TAIFA STARS YA MABORESHO YAINGIA KAMBINI BULYANHULU.



Kikosi cha Taifa Stars Maboresho kimeingia kambini jana (Desemba 1 mwaka huu) Bulyanhulu mkoani Shinyanga kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi itakayochezwa Desemba 9 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Ikiwa chini ya Kocha Mart Nooij, Stars Maboresho itapiga kambi mkoani humo hadi Desemba 6 mwaka huu ambapo itarejea jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa.
Wachezaji walioingia kambini ni Abubakar Ally (Coastal Union), Abubakar Ally Mohamed (White Bird), Aishi Manula (Azam), Andrew Vicent (Mtibwa Sugar), Atupele Green (Kagera Sugar), Edward Charles (Yanga) na Emmanuel Semwanda (African Lyon).
Gadiel Michael (Azam), Hashim Magoma (Stand United), Hassan Banda (Simba), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Joram Mgeveke (Simba), Kassim Mohamed Simbaulanga (African Lyon), Kelvin Friday (Azam) na Makarani Ally (Mtibwa Sugar).
Miraji Adam (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Muzamir Ally (Mtibwa Sugar), Omari Nyenje (Ndanda), Pato Ngonyani (Yanga), Rashid Mandawa (Kagera Sugar), Said Hamisi (Simba), Salim Hassan Mbonde (Mtibwa Sugar) na Shiza Ramadhan (Mtibwa Sugar).
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaishukuru kampuni ya kuchimba madini ya Acacia Mining PLC (zamani African Barrick Gold PLC) kwa kufadhili kambi ya Stars kupitia mgodi wa Bulyanhulu.

No comments:

Post a Comment