Mmoja wa
wanafunzi walioongoza mtihani wa Taifa wa darasa la saba mwaka huu mwenye umri
wa miaka 16 kutoka wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro anadaiwa kuozwa kwa
mwanaume mwenye umri wa miaka 50 baada ya wazazi wake kupewa sukari kilo mbili
kama mahari.
Kutokana
na hali hiyo, Mtandao wa Kuelimisha Jamii kuhusu Ukeketaji mkoani Kilimanjaro
(NAFGEM), umefanya jitihada za kumuokoa pamoja na wanafunzi wa kike wengine 15
waliotaka kufanyiwa vitendo vya ukeketaji kwa ngariba.
Msichana
huyo wa miaka 16 wa kabila la kimasai kutoka kata ya Orkolili (jina
limehifadhiwa) baada ya kufaulu mtihani huo, aliozeshwa kwa mmoja wa wanaume
ambaye ni wafugaji wa kabila hilo.
Meneja
Mipango wa Mtandao wa Kuelimisha Jamii kuhusu Ukeketeaji mkoani Kilimanjaro
(NAFGEM), Honoratha Nasua, alitoa taarifa za kuokolewa kwa wanafunzi hao katika
kijiji cha Naibili wilayani hapa.
“Wanafunzi
15 walikuwa wameandaliwa kwa ajili ya kukeketwa wakati wa mapumziko ya mwezi
Desemba, mwaka huu na waliamriwa kuacha shule ili waozeshwe baada ya
kukeketwa,” alisema.
Nasua
alisema katika utafiti huo wamefanikiwa kupata orodha ya Mangariba wanaohusika
katika mtandao wa ukeketaji.Alisema suala la mwanafunzi huyo aliyeozeshwa
limefikishwa katika Dawati la Jinsia la Polisi Wilaya ya Siha mkoani humo kwa
ajili ya kuchukua hatua zaidi za kisheria.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Dawati la Ukatili wa Kijinsia mkoa wa Kilimanjaro, Grace
Lyimo, alisema mwanafunzi huyo aliyeozeshwa aliokolewa baada ya polisi na
maofisa wa NAFGEM kuingilia kati.
Alisema
wazazi wa wanafunzi huyo wameshiriki kudidimiza maendeleo ya mtoto wao kwa
kukubali aolewe na kubuni mbinu mpya ya kukeketa watoto wachanga ili kukwepa
vyombo vya dola na mkono wa wanaharakati.
Chanzo:
Nipashe

No comments:
Post a Comment