SIMBA, MTIBWA ZAFIKIA ASILIMIA 90 ILI
KESSY ATUE ZAKE MSIMBAZI
Uongozi wa Klabu ya Simba umefunguka
kuwa, upo katika hatua za mwisho za kumalizana na beki namba mbili wa Mtibwa Sugar,
Hamis Kessy licha ya kuripotiwa kuwepo kwa ugumu wa mchakato huo wa usajili.
Hata hivyo
kumekuwa na taarifa kwamba mazungumzo yako katika hatua nzuri sana na pande
zote mbili, yaani Simba na Mtibwa Sugar zimekubali kwamba zimefanya mazungumzo.
Simba ambayo
imeshampa mkapata wa miaka mwili raia huyo wa Uganda, imekuwa katika mazungumzo
ya kumsajili Kessy licha ya kuwa Mtibwa imekuwa ikiweka ngumu, kuna uwezekano
wa kukubali kutokana na mchezaji mwenyewe kuonyesha nia ya kukubali dili.
Mwenyekiti wa
Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, alifunguka kuwa mazungumzo
yanaendelea vizuri na kama kila kitu kitaenda vizuri, kuna uwezekano wa usajili
huo kukamilika ndani ya siku chache zijazo.
Mkurugenzi wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser, alisema ni kweli
mazungumzo yanaendelea.
Wakati huohuo,
mchakato wa Simba kumuwania beki mwingine wa timu hiyo, Salim Mbonde,
umeendelea lakini dalili zinaonyesha kuwa Mtibwa imegoma katakata kumuuza
mchezaji huyo.
Taarifa kutoka Mtibwa zinaeleza kuwa klabu hiyo inahofia
kuuza wachezaji wake muhimu kwa kuwa ligi bado inaendelea, hivyo suala la
kumuuza mchezaji huyo kwa sasa wamelifuta rasmi.
Uongozi wa Simba umechukua uamuzi wa kusitisha kumsajili
mshambuliaji Danny Mrwanda wa Polisi Morogoro.
Simba imefikia
uamuzi huo baada ya kugundua hakusema ukweli kuhusiana na mkataba wake na
Polisi Morogoro.
Habari za
uhakika zimeeleza, Mrwanda hakuiambia Simba kama mkataba wake unamzuia kusaini
hapa nchini lakini unamruhusu kwenda nje ya Tanzania bila ya kipingamizi.
Mlinzi wa
kati Juma Nyosso amejiunga na kikosi cha Mbeya City Fc kwa mkataba wa mwaka
mmoja.Akizungumza mara baada ya kuisaini mkataba huo kwenye ofisi za timu zilizopo jengo la Mkapa Hall jijini Mbeya, Nyoso aliyewahi kucheza kwenye timu za Ashanti United, Simba na Coastal Union, alisema amekubari kujiunga na City kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa imani kuwa utatosha kuushawishi uongozi wa timu kumpa mkataba mrefu zaidi mara baada ya huu wa sasa.
Akiendelea
zaidi beki huyo aliyewahi pia kucheza kwenye kikosi cha timu ya
Taifa ‘Taifa Stars’ alisema kuwa mafanikio iliyopata Mbeya City
msimu uliopita yamekuwa sababu kubwa ya yeye kukubari kujiunga na City huku
akiamini kuwa amekuja kuongeza nguvu kwenye timu bora ili kuhakikisha mafanikio
ya msimu uliopita yanafanikiwa tena
.Kwa upande
wake Katibu Mkuu wa City Emmanuel Kimbe alimshukuru Nyosso kwa kukubari
kujiunga na timu hii huku akiamini kuwa uzoefu alionao mchezaji huyo utasaidia
kuimarisha safu ya ulinzi kwenye kikosi cha City.Kwa sasa Nyosso tayari yuko na
kikosi cha City kilichosafiri kwenda mjini Songea kwa ajiri ya michezo ya
kirafiki.

No comments:
Post a Comment