Akithibitisha kukamatwa kwa mtu huyo Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Tanga Fresser Kashai ameuambia mtandao huu kuwa mtuhumiwa amekiri
kufanya biashara hiyo ya bhangi kwa lengo la kujipatia kipato.
Kamanda Kashai amesema mtuhumiwa bado anashikiliwa na
jeshi la polisi na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayo mkabili baada ya
upelelezi wa awali kukamilika.
Jeshi la Polisi mkoani hapa linatoa wito kwa wakazi wa
jiji la Tanga kufanya biashara halali na kuacha kabisa biashara haramu za
uuzaji wa madawa yak kulevya kwa sababu yana madhara makubwa mtumiaji na vilevile
ni kinyume cha Sheria, na yeyote atakae bainika kujihusisha na Biashara hiyo
hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

No comments:
Post a Comment