Mabingwa
wa Tanzania bara wa mwaka 1988, Coastal union wameichapa kombaini ya Mombasa
magoli 3-1 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa
Mombasa Sport club jana.Katika mchezo huo maalum wa kujianda na mwendelezo wa ligi
kuu ya vodacom, kombain ya Mombasa walikuwa wa mwanzo kupata goli kupiti kwa
Makame Salim katika dakika ya 15 ya mchezo.Mkenya Ramadhani Salim aliisawazishia Coastal union katika dakika ya 32 na kupelekea kwenda mapumziko wakiwa sare ya goli 1-1.Katika kipindi cha pili Mkongoman Imbem aliiandikia Coastal union goli la pili katika dakika ya 46 na kurejea tena katika nyavu za kombaini ya Mombasa katika dakika ya 73 kwa mkwaju wa penati.
Mchezo huo ambao ni wa pili kwa kocha James Nyende Nandwa ulimalizika kwa Coastal union kuibuka na ushindi wa goli 3-1.Nandwa amejiunga na Coastal union kuchukwa nafasi ya Yusuf Chippo aliyejiunga na AFC Leopard kama kocha msaidizi.
Mchezo wa kwanza kwa Nandwa ulikuwa ni dhidi ya Mwadui FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania na mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.
No comments:
Post a Comment