HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Tuesday, 23 December 2014

MWAMUZI APIGWA MTAMA KWA KUMPA CHEZAJI KADI NYEKUNDU LIGI DARAJA LA PILI.



MWAMUZI aliyekuwa akichezesha pambano kati ya CDA na Milambo ya Tabora Steven Makuka kutoka Iringa amejikuta akikatwa mtama uwanjani katika mchezo wa ligi daraja la pili uliofanyika juzi kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.


Sakata hilo la aina yake lilitokea kipindi cha pili cha mchezo huo baada ya Mwamuzi kumwonesha kadi nyekundu mchezaji wa timu ya Milambo, Said Kantovu ambaye aliamua kumkata mtama baada ya tukio hilo hali iliyomfanya ayumbe kabla ya kupewa msaada na mwamuzi wa msaidizi Bakari Wiliam.
Kabla ya tukio hilo, mwamuzi huyo alimtoa nje kwa kadi nyekundu beki wa timu ya Milambo Rashid Shila kwa kumchezea rafu mshambuliaji wa timu ya CDA Ally Lutavi.

Hali hiyo ilisababisha wachezaji wa Milambo kumzonga mwamuzi kwa madai ya kutoridhishwa na namna alivyokuwa akichezesha mechi hiyo.

Mchezo huo ulihudhuriwa na mamia ya wakazi wa mjini hapa wakiongozwa na Diwani wa Kata ya Mnadani Steven Masangia ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika pambano hilo.
Katika dakika ya 43 mshambuliaji wa timu ya Milambo Nerdad Mrope alikosa bao la wazi baada ya kubaki na kipa wa timu ya CDA Francis Ishengoma. CDA walipata bao la kuongoza katika dakika ya 45 kupitia kwa kiungo wake Hussein Kunga.

Na hadi timu hizo zinakwenda mapumziko CDA walikuwa mbele kwa bao 1-0. Katika kipindi cha pili Milambo walifanya mabadiliko ya kumtoa Yusuph Jumanne na kuingia Abdalllah Ahmad huku CDA wakimtoa Abrahman Said na kuingia Shaka Titus lakini hadi mwisho wa mchezo huo CDA waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Milambo.

Baada ya mchezo kumalizika, kocha wa timu ya Milambo Kilindimya Athuman alimlaumu Mwamuzi kwa kuwatoa wachezaji wake kwa kadi nyekundu na kulitaka Shirikisho la Soka Nchini (TFF) kuachana na utaratibu wa kupanga waamuzi kutoka timu mwenyeji.

Kwa upande wake, kocha wa CDA, Juma Ikaba aliwapongeza vijana wake kwa kupata ushindi na kuahidi kuendeleza hilo katika mchezo unaofuata dhidi ya Ujenzi ya Rukwa. Kwa matokeo hayo CDA imefikisha pointi 7 katika michezo mitatu huku Milambo ikibaki na pointi zake nne.

No comments:

Post a Comment