Serikali imelifungia shindano la
Miss Tanzania kwa miaka miwili kutokana na sababu mbalimbali na ukiukwaji wa
taratibu walizojiwekea, ikiwemo udanganyifu mkubwa unaojitokeza kila mwaka
kwenye shidano hilo.
Maamuzi hayo yamechukuliwa na BASATA, ambapo Kaimu Mtendaji wa Baraza hilo Godfrey Mngereza amesema maamuzi hayo yalifikiwa baada ya kukaa kikao cha tathmini ambapo Kamati ya Miss Tanzania ilishindwa kujibu hoja za msingi za wadau na kukiri kuwepo udhaifu katika uendeshaji wa shindano hilo.
Maamuzi hayo yamechukuliwa na BASATA, ambapo Kaimu Mtendaji wa Baraza hilo Godfrey Mngereza amesema maamuzi hayo yalifikiwa baada ya kukaa kikao cha tathmini ambapo Kamati ya Miss Tanzania ilishindwa kujibu hoja za msingi za wadau na kukiri kuwepo udhaifu katika uendeshaji wa shindano hilo.
Tangu atangazwe aliyekuwa Miss
Tanzania 2014 Sitti Mtemvu mengi
yameongelewa kuhusiana na tetesi za udanganyifu wa umri na vitu vingine kadhaa
vinavyomhusu mrembo huyo ikiwemo suala la umri wake na kiwango cha elimu yake
ambapo yeye mwenyewe alikanusha taarifa hizo.
Novemba 8, 2014 Kamati ya Miss
Tanzania ilikutana na waandishi wa habari Dar es salaam na kutangaza kwamba Sitti Mtemvu ameandika barua kwa hiari yake yeye mwenyewe, kwamba
amelivua taji hilo hivyo kamati hiyo ikamtangaza Lilian Kamazima
aliyekuwa mshindi wa pili kushikilia taji hilo.
Maamuzi hayo yamechukuliwa na BASATA,
ambapo Kaimu Mtendaji wa Baraza hilo Godfrey Mngereza amesema maamuzi hayo yalifikiwa
baada ya kukaa kikao cha tathmini ambapo Kamati ya Miss Tanzania ilishindwa
kujibu hoja za msingi za wadau na kukiri kuwepo udhaifu katika uendeshaji wa
shindano hilo.
“Baada ya kupitia maelezo yote na
taarifa ya tathmini ya shindano hilo ni vyema tulisimamishe kwa muda ili
mwandaaji ajipange upya, atakaporejea arejee kwa nguvu na kuandaa shindano
lenye hadhi kubwa kuliko ilivyo hivi sasa…“– Mngereza.
Shindano hilo limekumbwa na kashfa
mbalimbali tangu mwaka 2006 ikiwemo ya kuvisha mataji warembo wasiokidhi
vigezo.
Chanzo cha Habari: Gazeti la Mtanzania, December
25.

No comments:
Post a Comment