| Viongozi wa UWAKA(Kutoka kushoto, Dr Slaa, Prof Lipumba & James Mbatia) |
WAKATI wananchi wakiwa bado
hawajalizika kuhusu Hatua alizochukua Rais Jakaya Kikwete Juu ya maamuzi
ya Bunge kuhusu ufisadi wa Zaidi bilioni 306 kwenye Akanti ya Tegeta
Escrow,kutokana na Rais Kikwete kulikejeri Bunge kwa kuyatupia mbali
mapendekezo mengi ya Bunge hilo.
Nao Umoja wa Vyama vya vikuu vya Upinzani nchini ambavyo vinaunda Umoja wa
Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA vimeibuka na kumvaa Rais Jakaya Kikwete na
kusema anahusika kwa kiasi kikubwa kwenye Ufisadi kwa kitendo chake cha
kumtetea Mmiliki wa wa kampuni ya Indepence power Solution limited , IPTL Bwana
Harbnder Singh (Singasinga)
Na Kusema
Umoja huo utaanzisha Maandamano nchi nzima kupinga Ufisadi huo ambao wanadai
unalindwa na Rais Kikwete kutokana na yeye kuhusika katika Wizi huo .
Kauli hiyo ya Vyama vikuu vya Upinzani vinavyounda UKAWA umetolewa leo
Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Umoja huo ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba wakati wa mkutano na
waandishi wa Habari ulioitishwa Mahususi ili kuzungumzia hutuba ya Rais Kikwete
kuhusu sakata hilo.
Profesa Lipumba alisema inasikitisha
kuona Rais Jakaya Kikwete ameacha kulitetea shirika la Umeme Tanesco na
kuwatetea Mataperi wa IPTL ambao wameliongizia hasara la mabilioni ya Fedha
shirika la hilo.
“Hutuba ya Rais kikwete imekuwa
mtetezi mkubwa wa Mmiliki wa PAP,anaacha kulitetea shirika la umma la
tanesco,harafu anadanganya umma kwa kiasi kikubwa kwamba pesa za IPTL si za
Umma hivi anashindwa hata kuelewa Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikal CAG
ambayo inaonyesha wazi kwamba wamiliki hawa wamefanya utaperi wa wazi
kabisa katika umiliki wake “
“Taarifa za mauzo ya
Kampuni ya Mechmar kwenda piper link kwenda PAP ziliwasilishwa katika taasisi
mbalimbali za Serikali na bwana Singh sote tunafahamu ni kughushi nyaraka ili
akwepe Kodi na hili ni kosa,hivi Kikwete alioni hili?”alihoJi Profesa Lipumba.
Profesa lipumba alizidi kusema hata Maazimio yanayotokana na Taarifa ya CAG
inayoonyesha wazi kuwa PAP siyo mmiliki wa halali wa wa hisa za Kampuni ya
Mechmar lakini Rais Kikwete hakuliona hilo.
Kwa Upande wake Katibu mkuu wa
Muungano vya hivyo wa Vya Upinzani vinavyounda UKAWA ambaye pia ni Katibu mkuu
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Dokta Wilbroad Slaa amesema Umoja
umepanga kuzunguka nchi nzima ikiwemo kuandaa maandamano kupinga kile
wanachodai Rais Jakaya Kikwete amewalinda wezi wa Ufisadi huo.
Dokta Slaa aliongeza kuwa Kitendo
cha Rais kikwete kuwatetea Wamiliki wa kampuni ya IPTL ni wazi Rais Kikwete
anahusiki kutokana na kuwepo kwa ushahidi way eye kuhusika na Wezi huo.
“Tunajua
wazi kwamba Rais kikwete kuhika na wizi huo kwani kunamtu mmoja anaitwa Guruma
ambaye katika watu waliopewa na bwana James Rugimalira jina lake limetajwa
kupokea mabilioni ya Fedha na mtu huyo mimi namfahamu sana,Bwana Guruma
anajulikana sana ni msimamizi wa Miradi ya Rais kikwete na leo kachukua pesa za
Escrow unategemea nini hapa na ndio maana anasuasua kuwachukulia hatua wamiliki
wa IPTL”Alisema Dokta Slaa.
Aidha,Dokta Slaa alisema kitendo cha Ufisadi huo kutoke na Idara ya
Usalama wa Taifa kushindwa kulinda nchi kwenye ufisadi huo ni wazi idara
hiyo imeshindwa kazi.
“Usala wa Taifa
upo kila Barozi inashangaza sana kuona Idara hii inashindwa kuona utaperi wa
mmiliki wa IPTL au tutegemee nini ndio maana hata kwenye Ufisadi wa EPA,tuliona
Jinsi Kampuni iliyokuwa ikimilikiwa na Ofisa wa Usalama wa Taifa ilivyochota
pesa unategemea nini”
“Na hata alivyosema mara baada ya kutua uwanja wa ndege alipotoka
kutibiwa anavyosema alijui sakata hili kutokana na yeye kuh umwa, ni
kuwadanganya watanzania kwani baada ya masaa mawili kutoa uwanja wa ndege hapo,niliona
email aliyekuwa akitumiana na bwana Rugimalira,sasa huyo ni kiongozi
kweli”alihoji Dokta Slaa.
Naye Mwenyekiti wa chama cha NCCR
Mageuzi James Mbatia alisema ni Rais kikwete amekosa maamuzi katika nchi
kutokana na ktendo chake cha kushindwa kuwachukulia hatua waliohusika na kusema
pesa za wananchi zimepotea huku taifa likiosa fedha hususani wao wabunge
mapaka sahivi hakuna hata mbunge aliyepata hata mshahara.
Umoja huo wa UKAWA ni muunganiko wa Vyama vya CHADEMA,CUF na NCCR pamoja NLD.
No comments:
Post a Comment