Wananchi mkoani Tanga wametakiwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuimarisha usalama kwa nyakati hizi za Sikukuu za Krismasi na mwaka mpya.
Wito huo umetolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga Frasser Kashai wakati alipokuwa akitoa taarifa ya mikakati ya Jeshi la Polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama wakati wa sikukuu hizo .
Kamanda Kashai alisema Jeshi hilo limejipanga kuimarisha Doria za magari, pikipiki na watembea kwa miguu katika maeneo yote ya jiji hilo kwa kuzingatia taarifa za kiintelejensia na kuimarishwa ulinzi katika nyumba za ibada ,kumbi za starehe ,fukwe za bahari(BEACH) na maeneo yote yenye msongamano wa watu wengi .
Aidha alisema katika barabara zote kutakuwa na Askari wa kutosha wa usalama barabarani ili kuhakiksha sheria za barabarani zinazingatiwa ipasavyo lakini linaendelea kuimaisha check ponti zote zilizopo barabarani zinazotoka nakungia katika Mkoa wa Tanga.Sambamba na hilo aliawasa viongozi wa vitongoji ,mitaa na Kata kuwabaini vijana wanaofanya vitendo vya kihuni na kuhamasisha vikundi vya ulinzi shirikishi vilivyopo kwenye maeneo yao kuimarisha ulinzi katika maeneo hayo.
Hata hivyo Kamanda Kashai aliwataka wazazi na walezi kuimarisha ulinzi katika familia pamoja na nyumba zao hususani uangalizi kwa watoto wadogo ili kuwaepushia ajali mbalimbali ikiwa na kupotea.
No comments:
Post a Comment