HIKI NI KILIO CHA LULU KWA
WATAYARISHAJI FILAMU NCHINI.
Amesema jambo hilo, linampa hofu
kuwepo kwa upendeleo kwa wasanii wapya kuliko, wakongwe.
“Waongozaji a filamu ni wachache,
naweza kusema ni wale wale, kila siku wasanii wazuri wanaibuka, wanaonyesha
uwezo mkubwa,”alisema Lulu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam,
Lulu ameonyesha hofu kuwa, wasanii wakongwe, akiwemo yeye kukosa nafasi kama
ilivyokuwa zamani.
“Waongozaji wa filamu ni wachache,
naweza kusema ni wale wale, kila siku wasanii wazuri wanaibuka, wanaonyesha
uwezo mkubwa,”alisema
Lulu alisema hiyo ndio moja ya
sababu inayofanya wasanii wengi kutengeneza filamu zao wenyewe kama waongozaji,
watayarishaji wakuu baada ya kukosa nafasi mara kwa mara.
Hivi karibuni, Lulu alitoa filamu
aliyoiandaa mwenyewe ya ‘Mapenzi ya Mungu,’ ambayo amemshirikisha mama wa
marehemu, Steven Kanumba.
KAJALA SASA ATAMBA
KWA KIMYA CHAKE KINA MSHINDO.
Muigizaji wa filamu nchini, Kajala
Masanja amesema ukimya wake, utaibua kishindo kizito baadae.
Amesema hivi sasa, ameupa kisogo
uigizaji, anafanya biashara zingine kwa ajili ya kumuingizia mapato.
Akizungumza jijini Dar es Salaam,
Kajala alisema kamwe hawezi kuacha uigizaji, licha ya baadhi ya watu kusema
‘amefulia.’
“Bado kuna mambo yangu nafuatilia,
siwezi kufanya kazi moja tu, filamu pekee bila shughuli zingine, huwezi kutoka
kimaisha,” alisema Kajala.
Aliwataka mashabiki wake, kuwa
tayari, anajiandaa kuachia kazi ya kufungia mwaka 2014.
“Wakae mkao wa kula, naandaa kazi
nzuri, naamini wataipenda, watakapoiona.”
IDRIS KUSAKAHESHIMA KWANZA, SIYO
FEDHA.
“Kwa kweli, sijafurahia fedha
kabisa, najivunia heshima niliyopewa na watanzania wenzangu, wameniwezesha kwa
kura baada ya kuona nafaa,” alisema Idris Sultan.
Mshindi wa shindano la Big Brother
Africa, Idris Sultan amesema hafurahii fedha alizopata, bali heshima aliyopewa
na watanzania.
Sultan, aliwabwaga wenzake na
kujinyakulia kitita cha dola 300,000 (Zaidi ya sh. milioni 480) baada ya kuishi
kwenye jumba la BBA kwa siku 63.
Akizungumza jijini Dar es Salaam,
Sultan, alisema kwamba ushindi huo, umedhihirisha namna watanzania wenzake,
wanavyompenda na walivyokuwa bega kwa bega naye.
“Kwa kweli, sijafurahia fedha
kabisa, najivunia heshima niliyopewa na watanzania wenzangu, wameniwezesha kwa
kura baada ya kuona nafaa,” alisema Sultan.
Aidha, Sultan alisema hakutarajia
kushinda, kutokana na changamoto zilizokuwepo ndani ya jumba.
“Shindano lilikuwa gumu, watanzania
ndiyo wameniwezesha kuibuka mshindi. Wamenipa heshima kubwa,” alisema Sultan.
SHETTA ASEMA MASHABIKI HAWATAFURAHI
ASIPOPIGA HATUA.
“Nchi kama Afrika Kusini ambayo, nimeamua
kuwatumia watayarishaji video wa huko, kuna uwezekano mkubwa wa kutengeneza
uhusiano wa kimataifa na wasanii wakubwa, sidhani kama wapenzi wangu watafurahi
kuniona, niko pale pale, sipigi hatua,” alisema Shetta.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,
Nurdin Bilal a.k.a Shetta, amesema hadhani kama mashabiki wake, watafurahi
kumuona hapigi hatua ya kufanikiwa kimuziki.
Shetta, amesema kutokana na hilo,
ndiyo sababu ya kuchanganya vionja vya nchi mbalimbali, anaporekodi video za
nyimbo zake.
Akizungumza jijini Dar es Salaam,
msanii huyo, alisema mazingira ya Afrika Kusini, amekuwa akiyatumia kunogesha
kazi zake.
Alisema bila kufanya hivyo,
mashabiki watashindwa kumuelewa, hivyo amekuwa akijenga uhusiano mzuri wa
kimataifa, kwa lengo la kufika mbali.
“Nchi kama Afrika Kusini ambayo,
nimeamua kuwatumia watayarishaji video wa huko, kuna uwezekano mkubwa wa
kutengeneza uhusiano wa kimataifa na wasanii wakubwa, sidhani kama wapenzi
wangu watafurahi kuniona, niko pale pale, sipigi hatua,” alisema.

No comments:
Post a Comment