Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Fresser Kashai akizungumza na waandishi
wa Habari.Kushoto ni mwandishi wa Mtandao huu Rebeca Duwe
|
Na.Rebeca Duwe TANGA
Mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la Omari Bakari 31 mkazi wa Maguzoni alifariki dunia
baada ya kupigwa ngumi na Shabani Zuberi 19 Mnyakyusi mkazi wa Maguzoni.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Frasser Kashai amesema
tukio hilo limetokea mnamo tarehe 4 Novemba mwaka huu majira ya saa 6 mchana
maeneo ya Maguzoni kata ya Kwafungo Tarafa ya Bwembwela Wilayani Muheza.
Aidha
Kamanda Kashai amesema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi na mtuhumiwa
amekamatwa na atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika muda wowote
kuanzia sasa.
No comments:
Post a Comment