Na Rebeca Duwe .TANGA
Jeshi la polisi
linawashikilia raia 9 wote wanaume kutoka nchini Ethopia wakiwa wameingia
nchini bila kibali raia hao ni 1. Basido Habibi 35, 2.Markos Wernecho 25,
3.Zeleki Riganoho 22, 4.Nurdini Sule 26, 5.Zeleki Marasha 22, 6.Erigo Maresa
22, 7.Abtiman Nurama 27, 8.Tariku Oswai 23 na 9.Abraham Hasafa 28.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani hapa Frasser Kashai amesema
tukio hilo limetokea mnamo tarehe 4 novemba mwaka huu majira ya saa 6:30 huko
Mjesani Getini Kata ya Mnyenzani Tarafa ya Maramba Wilaya ya Mkinga.
Baadhi ya
bodaboda wa Mji wa Pongwe kwenye kituo cha daladala za Tanga- Pongwe
|
Sambamba
na hayo Kamanda Kashai amesema watuhumiwa hao walikuwa wamepakiwa kwenye
pikipiki 3, ambazo ni T.551 CTR aina ya Yamaha iliyokuwa ikiendeshwa na
Athumani Soma 34 , 2.T.159 AUP aina ya Watco iliyokuwa ikiendeshwa na Singano
Hamisi 22 na 3.T.751 CDT aina ya Fekon iliyokuwa ikiendeshwa na Tito John 45 wote
wakiwa ni wakazi wa Pongwe wakiwatoa
Maramba kwenda Pongwe.
Katika tukio
jingine
jeshi la polisi linawashikilia watuhumiwa 3 raia wa Ethopia ambao waliingia
nchini bila kibali raia hao ni 1.Nukse Kanji 2.Mohamed Samali na 3.Sultani
Abdallah.
Kamanda
wa polisi mkoani hapa Frasser Kashai amesema tukio limetokea mnamo tarehe 4
novemba mwaka huu majira ya saa 11 jioni huko Horohoro mpakani Wilaya ya
Mkinga.
Pia
Kamanda Kashai amesema watuhumiwa wote wamekamatwa na watafikishwa mahakamani
kujibu shtaka linalowakabili
Jeshi la polisi
linaendelea kuwasisitizia kutoa taarifa fiche za uwepo wa wahalifu na uhalifu
katika maeneo wanayoishi na zitafanyiwa kazi kwa usiri mkubwa na kuhakikisha
watuhumiwa hao wanakamatwa na kufikishwa mahakamani.
No comments:
Post a Comment