RAIS WA TFF JAMAL
MALINZI
|
Michuano ya Ligi
Daraja la Pili (SDL) inayoshirikisha timu 24 katika makundi manne ya timu sita
sita kwa mtindo wa nyumbani na ugenini inaanza kutimua vumbi Novemba 22 mwaka
huu ambapo Mpanda United itakuwa mwenyeji wa Ujenzi Rukwa, taarifa kutoka TFF
imeeleza.
Mechi
hiyo ya kundi A itachezwa kwenye Uwanja wa Mandela mjini Sumbawanga.
Siku hiyo
hiyo katika kundi hilo kutakuwa na mechi kati ya Mvuvumwa FC na CDA (Lake
Tanganyika, Kigoma), na Milambo dhidi ya Singida United kwenye Uwanja wa Ali
Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Kundi
B mechi za ufunguzi ni kati ya Pamba na JKT Rwamkoma kwenye Uwanja wa CCM
Kirumba huku Bulyanhulu FC ikiwa mwenyeji wa AFC kwenye Uwanja wa Bulyanhulu
mkoani Shinyanga.
Abajalo
FC ya Dar es Salaam itaikaribisha Kariakoo FC ya Lindi kwenye mechi ya kundi C
itakayochezwa Uwanja wa Karume. Nazo Kiluvya United na Transit Camp
zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani.
Kundi
D mechi tatu za ufunguzi ni kati ya Town Small Boys na Volcano FC (Uwanja wa
Majimaji, Songea), Njombe Mji na Mkamba Rangers (Uwanja wa Sabasaba, Njombe),
na Wenda FC dhidi ya Magereza Iringa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
No comments:
Post a Comment