HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Thursday, 20 November 2014

WATATU WAKAMATWA NA DOLA 11200 BANDIA ZA KIMAREKANI TANGA




Kamanda wa Polisi mkoa wa TANGA
Kamishna mwandamizi msaidizi wa Polisi SACP, Frasser Kashai
Akionesha noti bandia kwa waandishi wa habari.
Jeshi la polisi mkoani Tanga linawashikilia watu watatu kwa kosa la kupatikana noti bandia 112  ambazo ni Dola za kimarekani ambazo kama zingekuwa ni za halali zina thamani ya dola za kimarekani 11,200 ambazo ni sawa na milioni 20 kwa fedha za kitanzania .

Watuhumiwa hao Julius Kanza 30 mkazi wa Ubongo, Kenedy Binaga 35 mkazi wa Sinza, na Ramadhani Saddy 33  mkazi  wa Mwenge walikamatwa wakiwa na gari yenye Chasis namba JLg 100037726.

Akizungumza na wandishi wa habari  kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, Kamishna mwandamizi msaidizi SACP, Frasser Kashai  kuhusiana na tukio hilo amesema limetokea Novemba 17 mwaka huu majira ya sa 7:30 mchana  maeneo ya barabara ya 16 Kata na Tarafa ya Ngamiani Kati  Wilayani Tanga.

Aidha watuhumiwa hao wamekiri kufanya biashara hiyo ya uuzaji wa fedha bandia. Wote wamekamatwa na watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinayo wakabili baada ya upelelezi wa awali kukamilika.

Wakati huo huo,Jeshi la Polisi Mkoani Tanga linaendesha msako mkali wa kuwatafuta wahusika wa matukio ya mauaji ya Mkulima mmoja yaliyotokeaKijiji cha Nyadigwa Kata na Tarafa ya Kimbe wilayani Kilindi.

Kamanda Kashai alisema kuwa tukio hilo la mauaji hayo lilitokea Novemba 18 mwaka huu majira ya saa kumi na moja na dakika arobaini na tano katika eneo la kijiji cha Vyadigwa Kata ya Kimbe wilayani humo.

Akizungumzia tukio hilo,Kamanda Kashai alisema mkulima wa Vyadigwa alikutwa porini akiwa amejeruhiwa maeneo ya utosini kwa kitu chenye ncha kali na watu wasiojulikana hali iliyomsababishia kifo chake.

Alisema kuwa mkulima huyo alifariki dunia saa kumi jioni wakati akiwakwenye hospitali Teule ya wilaya ya Kilindi (KKKT) ambapo chanzo cha mauaji hayo bado kinachunguzwa

No comments:

Post a Comment