Hivi
Karibuni nilijikuta ktk wakati mgumu pale nilipoombwa Ushauri na Rafiki Yangu
wa Karibu ambaye alinisimulia mkasa huu wa kweli ambao unamkuta na bado unamkabili
mpaka sasa.

Anaye
mpenzi ambaye walikutana zaidi ya miezi mitano sasa, kabla ya kuanzisha
mahusiano kila mmoja alikuwa na yake ya kumshawishi mwenzie ambapo yeye
alimweleza BINTI kuwa anampenda kwa
dhati na hakuwa na mpenzi kwa wakati huo, lakini hakusita kumueleza ukweli
kuhusu hali yake ya kuichumi kuwa hana pesa sana ila anajimudu kwa mahitaji ya
maisha na hata vingine vidogo vya starehe, binti nae akasema hana Mpenzi kwani
alitendwa mara kadha hivyo akaona bora ajiweke pembenia na Mapenzi ili
kumsubiri alie chaguo lake na zaidi akamhakikishia kuwa anampenda, hajali pesa
na angependa amkute analala chini ili wanze pamoja ujenzi wa familia kwani wote
wana lengo la kuonana baadae.
Anapoeshi BEST yangu ni mbali na BINTI kwani ni mkoa mmoja kwa mwingine,
kama ilivyo vijana hupenda kusalia nyumbani na wazazi mpaka pale apatapo mwenza
au mtu wa kumshawishi kuwakimbia wazazi, hivyo BEST alikuwa bado anaishi na wazazi.
BINTI akawa anamtembelea kwa vipindi kadhaa
huku Mapenzi yakinoga kiasi wakafikia hatua nzuri ya uchumba rasmi ambapo binti
alitambulishwa kwa wazazi wa BEST.
BEST hakuishia hapo akahakikisha
anafanikisha barua ya uchumba na hatima akafahamishwa wa wakweze kuwa
amekubaliwa na mahari pia akatajiwa, hivyo mipango ya kuitafuta ikaanza.
Kufikia
hapo BINTI akawa anamshawishi BEST atoke kwa wazazi ili
anapomtembelea afikie kwake, wazo ambalo BEST
alilipokea na kulitekeleza, sasa akapanga chumba.
Lakini
wakati huohuo anapaswa kutafuta mahari, gharama za harusi, gharama za kodi ya
pango kila mwezi, umeme na maji matumizi yake yeye n.k
Lakini
BINTI nae akaibuka na jipya kuwa
anahitaji kutumiwa pesa ya matumizi, tena BEST
awe anatuma pasipo kuombwa jambo ambalo alilipokea na kuanza kutekeleza
japo kwa 50% hakumudu kwani alipoombwa 10000 alituma 5000.
Migongano
isiyokuwa na msingi ikaibuka na hata kufikia hatua kuhatarisha mahusiano
yao.Kwa kuwa BEST amependa aliamua
kuwa mpole kwa kila kitu ili asimkose ampendae, akawa ni wakuomba msamaha na
kujishusha kila mara pale wanapokosana.
Sasa
imekuwa Mateso na Maumivu kwani Mapenzi yamepungua sana, BEST ameacha kuongea na watu wote usiku ili aongee na binti lakini
akimpigia simu BINTI hana cha
kuongea, mchana anapiga BINTI
anajibu majibu ya mkato, maneno kama bby, honey, “I mic u”,mchumba
yamesahaulika, Wakati hapo kabla simu zilikuwa zinagongana hewani kila mmoja
nampigia mwenzie, wanakaribishana kula, kila sms haikosi neno bby au kuishia na
I LOVE U,
Ule
utani wa Wapenzi umekufa na cha kusikitisha BINTI hana mpango wa kumtembelea BEST kwa muda sasa kwa madai yuko bize.Mbaya zaidi binti anamdharau,
hamjali na kama Best asipopiga simu BINTI
hata kubeep hajaribu.Lakini bado BEST
anapenda zaidi na zaidi. *Nimejaribu kutafakari kuwa huenda Pesa ni tatizo
lakini bado sijapata jibu la uhakika*

SASA BEST AMEKONDA KWA MAWAZO, NIKIMTAZAMA NI KAMA
ANAUMWA..!
AMEKUJA ANAOMBA NIMSHAURI JE.! WAUNGWANA NIANZIE WAPI.????
No comments:
Post a Comment