Jeshi la polisi
mkoani hapa linawashikilia watu sita kwa kosa la kuingia nchini bila
kibali. Watu hao wamekamatwa wakitokea
Muheza kuelekea Dar es salaam ambapo wanne kati yao ni raia wa Ethiopia na wawili nai
ni raia wa Somalia .
Akithibitisha
kukamatwa kwa wahamiaji hao haramu kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa
Frazzer Kashai amesema raia hao walikamatwa manamo tarehe 13 novemba mwaka huu
majira ya saa kumi na mbili asubuhi huko katika kizuizi cha Polisi Kabuku Kata
ya Kabuku na Tarafa ya Mzundu Wilaya ya Handeni wakiwa wana safiri na basi la
kampuni ya Raha leo lenye namba za usajili T 795 ATJ Likitokea Muheza kuelekea
Dar es salaam.
Aidha
Kamanda Kashai amewataja kwa majina watu hao kuwa ni Desanap Aye 21, Tesua
Wonder 23, Malee Sami 30,na Elimias Tamasgen25 wote raia wa Ethiopia, na
wengine wakiwa ni Shafii Mohamedi 23,na
Abnur Mohamedi 25 wote wakiwa ni raia wa
Somalia.
Hata
hivyo Kamanda ameongezea kwakusema kuwa watuhumiwa wamekamatwa na watafikishwa
mahakamani baada ya upelelezi wa awali kukamilika.
No comments:
Post a Comment