Kamanda Kashai
|
Mnamo tarehe 13
novemba mwaka huu majira ya saa 10:30 asubuhi huko maeneo kata na Tarafa ya
sindeni wilaya ya Handeni Menyemo Moilo
Lengeke mwenye umri wa miaka 20 alikutwa
amekufa maji wakati akiogelea kwenye bwawa la maji na imeelezwa kuwa Chanzo cha kifo hicho ni
kunasa kwenye matope chini ya bwawa .
Katika
tukio jingine manamo tarehe 12 novemba mwaka huu majira ya saa 17:00 jioni
maeneo ya kitongoji cha Gombelo Kijiji cha Kwamnele Kata ya Ndolwa na tarafa
ya Mzundu Amina Selemani Kopwe (35 )
mkulima na mkazi wa Kwamnele alikutwa amejinyonga juu ya mti hadi kufa kwa kutumia
kitenge ambacho alikuwa amekifunga juu ya mti huo umbali wa mita 60 toka nyumba anayoishi.
Aidha
imebainika kuwa kabla ya kufanya tukio hilo marehemu alikuwa anasumbuliwa kwa
muda mrefu na maradhi ya ugonjwa wa
UKIMWI jambo lililo mfanya kukata tama ya kuishi na hata kufikia uamuzi wa
kujinyonga.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga Fresser Kashai amesema
baada ya tukio hilo dada wa marehemu aitwaye zuhura
Selemani mwenye umri 44 ambaye
alikuwa anamuuguza marehemu kwa muda mrefu alikwenda kutoa taarifa Polisi juu
ya kutokea kwa tukio hilo.
Mwili
wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwaajili ya mazishi baada ya
uchunguzi wa Daktari kukamilika.
No comments:
Post a Comment