Jeshi la polisi mkoani hapa linawashikilia watu watatu
ambao wamekamatwa na magunia mawili ya bangi
katika ofisi ya mabasi ya kampuni ya Simba Mtoto yenye uzito wa kilo 100 ambayo thamani yake
bado haijajulikana .
Akithibitisha kutokea
kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani hapa Frasser Kashai amesema tukio hilo limetokea mnamo
tarehe 12/11/2014 majira ya saa mbili asubuhi kwenye kituo cha basi kilichoko
kata ya Ngamiani tarafa ya Ngamiani Kati Wilaya ya Tanga.
Kamanda Kashai
amesema watuhuhumiwa hao ni 1. Hawa
Athumani 37 mfanya biashara na mkazi wa duga 2.Hilda Julius 24 mfanyi biashara na mkazi wa Donge 3.Ayubu
Uledi 29 mfanyibiashara na fundi wa
magari mkazi wa Mabawa na wote watatu wamekamatwa na watafikishwa mahakamani
baada ya upelelezi wa awali kukamilika.
No comments:
Post a Comment