“Kwanza nilipata
tatizo la presha ambayo ilisababisha miguu kuvimba lakini sikuwa na shaka kwani
nilijua ni hali ya kawaida kwa mama mjamzito kuvimba miguu kisha hurejea katika
hali ya kawaida. “Baada tu ya kujifungua, mguu mmoja ulirudi kama kawaida
lakini huu (wa kushoto) ukawa bado, nilipokwenda hospitali waliniambia nisijali
utarudi wenyewe kama zamani. “Wakaniambia niendelee kunywa vidonge vya Laxis
walivyonipa kwa ajili ya kupunguza maji. “Lakini cha ajabu, siku moja hali
yangu ilizidi kuwa mbaya, nikaenda Hospitali ya Temeke. Wao walishindwa
kunitibu na kunihamishia Muhimbili ambako nililazwa kwa muda wa siku tano,”
alisema
Bi Asna alivyo hivi sasa
|
Aliongeza
kuwa, baada ya kuruhusiwa kurejea nyumbani, alianzishiwa kliniki ya ugonjwa wa
matende iliyopo Muhimbili lakini katika hali ya kusikitisha madaktari walimwambia
hawezi kutibiwa nchini. “Kwa kweli nililia kwa uchungu maana nilijua uwezo wa
kwenda huko nje ya nchi sina, nikaona nakufa na urembo wangu.” Kwa upande wake,
Disnia alisema yeye pia aliupata ugonjwa huo mwaka 2004. Kwanza alihisi maumivu
ya kichwa ghafla usiku huku mwili ukitoka jasho. Asubuhi kulipokucha, alikuta
mwili umevimba. “Nilichukuliwa hadi Hospitali ya Bombo.
Bi. Asna Kabla hajapatwa na maradhi hayo
|
Pale
nililazwa kwa siku saba, presha ilikuwa juu, nikawekewa dripu, nilichomwa
sindano presha ikashuka. Uvimbe wa mwili ukapungua isipokuwa mguu huu wa
kushoto, madaktari waliniruhusu kurudi nyumbani ili nianze kliniki,” alisema.
Alisema pamoja na kuanza kliniki, hali ikazidi kuwa mbaya. Amezunguka hospitali
nyingi na kutibiwa, lakini kote huko imeshindikana hadi alipoambiwa asingeweza kutibiwa
nchini na anatakiwa kuwa na fedha kiasi kisichopungua shilingi milioni 20.
No comments:
Post a Comment