TIMU ya Coastal Union ya Vijana U-20 imepania
kuhakikisha inatetea taji lake wanalolishikilia la Michuano ya Kombe la Uhai
kwa kufanya vizuri katika mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuanza hivi
karibuni hapa nchini.
Coastal Union U-20 ambao ni mabingwa wa kombe hilo
mara baada ya kuifunga Yanga kwenye mechi ya Fainali ya Mashindano hayo msimu
uliopita kwenye mchezo fainali ambao ulichezwa uwanja wa Chamazi Jijini Dar es
Salaam.
Ubinde amesema kuwa kwenye mashindano hayo msimu huu
timu hiyo itaingia ikiwa na lengo moja la kuhakikisha wanapambana kufa na
kupona ili kuweza kuendeleza kushikilia ubingwa wake kwa sababu ya uimara wa
kikosi hicho.
Amesema kuwa hatuendi kushindana kwenye
michuano hiyo bali kuhakikisha tunatetea taji letu la Ubingwa wa Michuano hiyo
ambao sisi tunaingia kama mabingwa watetezi.
Ameongeza kuwa kikosi cha timu hiyo kimeimarika
vilivyo na kipo tayari kushiriki mashindano hayo kwa mafanikio kutokana na kuwa
na wachezaji mahiri wenye uwezo wa kuleta mapinduzi kwenye michuano hiyo.
Kikosi hicho kinaundwa na wachezaji nguli akiwemo
mlinda mlango namba mbili wa kikosi cha Coastal Union inayoshiriki
ligi kuu Fikirini Suleiman “Mapara”Mohamed Twaha “Dijong”,Mtenje Albano na
Mohamed Omari “Hungry”
Meneja huyo amesema kuwa wachezaji wa timu hiyo wapo
kwenye morali wa kuhakikisha wanafanya vizuri kwa kucheza kwa umakini mkubwa
lengo likiwa kupata matokeo mazuri kila mechi watakayocheza.
No comments:
Post a Comment