CITY BADO INA NAFASI YA
SKUHINDA TAJI LA LIGI KUU - PELLEGRINI.
MENEJA wa klabu ya Manchester City, Manuel Pellegrini bado ana uhakika
wa kutetea taji la Ligi Kuu pamoja na kupitwa kwa alama nane na vinara Chelsea.
City ambao watakuwa wenyeji wa Swansea City leo baada ya mapumziko kupisha
mechi za kimataifa kumalizika, wamefanikiwa kushinda mechi moja kati ya sita za
mashindano yote walizocheza hivi karibuni.
Kiwango cha timu hiyo katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya pia
imekuwa ya kusuasua huku wakiwa katika hatari ya kushindwa kuvuka hatua ya
makundi. Hata hivyo Pellegrini bado amekuwa na imani na kikosi chake kufanya
vyema katika ligi ya nyumbani na Ulaya msimu huu.
Pellegrini amesema sasa sio wakati wa kuangalia
yaliyotokea nyuma kwani bado kuna mechi nyingi za kucheza katika ligi na Ulaya.
Kocha huyo aliongeza kuwa bado kuna mechi 27 hivyo kuna alama zaidi za
kupigania hivyo wataona itakavyokuwa mpaka mwishoni mwa msimu.
SAMMER AONGEZWA MIAKA MITATU
BAYERN.
KLABU ya Bayern Munich imetangaza kumuongeza mkataba wa miaka mitatu
zaidi mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo Matthias Sammer ambao utamalizika
mwaka 2018.
Sammer ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani na
kocha, alijiunga na Bayern mwaka 2012 akitokea Shirikisho la Soka la Ujerumani
ambako nako alikuwa mkurugenzi wa michezo.
Akihojiwa na wanahabari Sammer amesema miaka
miwili na nusu ambayo ameitumikia klabu hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kwani
walifikia malengo yao mengi waliyojiwekea.
Toka atue Bayern, Sammer
amefanikiwa kuisaidia timu hiyo kushinda taji la Bundesliga katika msimu wa
2013-2014, Kombe la Ligi sambamba na taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya 2013.
WENGER AMUITIA THIERRY HENRY DILI LA UKOCHA ARSENAL
GWIJI
wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry anaweza kurejea katika klabu hiyo kwa mara
ya tatu, lakini safari hii kama kocha si mchezaji tena, amesema Arsene Wenge.
Henry’
anamaliza Mkataba wake katika klabu ya New York Red Bulls mwezi ujao mwishoni
mwa msimu wa Ligi Kuu ya Marekani, MLS na ingawa hajatangaza kama atastaafu,
lakini wengi wanaamini utakuwa mwisho wake wa kucheza.
Henry
amewahi kusema angependa kuifundisha Arsenal, wakati anachezea klabu hiyo
katika miaka yake minane, ambayo alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu na kuwa
mfungaji bora wa kihistoria wa klabu kabla ya kutimkia Barcelona mwaka 2007.
Alirejea
kwa muda kwa mkopo kutoka New York Januari mwaka 2012 na alifunga jumla ya
mabao 228 katika klabu hiyo ya Kaskazini mwa London.
No comments:
Post a Comment