Bio Bus,lenye
viti 40 na ambalo linatoa huduma ya uchukuzi kati ya Bath na uwanja wa ndege wa
Bristol ,linaweza kusafiri hadi maili 186 kwa kutumia tangi moja la gesi.
Gesi hiyo
hupatikana kupitia kutibu maji taka na uchafu wa chakula usiofaa kwa matumizi
ya binaadamu.
Uchafu
unaopatikana katika abiria wa basi moja unaweza kutumiwa kutoa kawi ya
kulisafarisha basi hilo kutoka Lands End hadi John O'Groats.
Basi hilo ambalo
limepewa majina kadhaa ya kutungwa likiwemo lile la Basi la pili linapongezwa
kama njia mojawapo ya kuchochea usafiri wa uma huku ukiimarisha ubora wa hewa
jijini.
Gasi inayotumiwa
kuliendesha gari hilo hutoka katika mradi wa maji taka wa Bristol ambao
husimamiwa na GENeco ambyo ni kampuni tanzu ya Wassex Water.
Mohammed
saddiq,meneja mkurugenzi wa kampuni ya GENeco ,anaamini chakula na maji taka
yanaweza kutoa kawi ya Biomethane inayotoa gesi katika shirika la kitaiafa la
gesi inayoweza kutoa gesi yenye uwezo wa kutumika katika nyumba 8,500 mbali na
kuliendesha basi hilo la Bio.


No comments:
Post a Comment