MASHINDANO ya Shimuta yamezinduliwa leo ramsi na Mkuu wa wilaya
ya Muheza Subira Mgalu ambapo alizitaka mashirika yanayoshiriki mashindan o
hayo kuhakikisha wanazingatia taratibu za michuano hiyo kwa kuchezesha
wachezaji ambao watakuwa wafanyakazi na sio vyenginevyo.Mashindano hayo yanashirikisha timu 20 ambazo ni Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC),Chuo Kikuu Huria(OUT),Chuo cha Elimu ya Biashara(CBE),Kampasi za Mbeya na Dar es Salaam na Mwanza,Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO),Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM),Chuo Kikuu cha Ardhi.
Timu nyengine ambazo zinashiriki mashindano hayo ni Hifadhi ya Taifa Tanzania(TANAPA),Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini(IRDP),Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma(CDA),Chuo Kikuu cha Mzumbe,Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi(MOCU),Chuo kkikuu cha Muhimbili cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS),Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Kauli mbiu ya Mashindano hayo msimu huu ni "Michezo kuboresha Afya za
Wafanyakazi "Tufanye Michezo sehemu za Kazi.
CHANZO:TANGA RAHA BLOG
No comments:
Post a Comment