Real Madrid imekubali
kuuondoa msalaba ulio kwenye nembo yake baada ya kupata udhamini mpya Uarabuni.
Klabu hiyo tajiri duniani
imepata udhamini mnono na Benki ya Abu Dhabi inayojulikana kama National Bank
of Abu Dhabi.
Hali hiyo imefanya Madrid
iondoe msalaba ulio juu kabisa ya nembo yake katika nembo zote zitakazotumika
kwenye Falme za Kiarabu.
Hiyo inatokana na imani ya
Kiislamu na ndiyo dini kuu kwa Falme za Kiarabu (UAE) yenye emirates maarufu na
miji mikubwa zaidi ni Dubai na Abu Dhabi.
No comments:
Post a Comment