Rais wa Tanzania
Jakaya Mrisho Kikwete alifanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika
Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland nchini
Marekani.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania, Rais
Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia uchunguzi wa
afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji matibabu ya aina hiyo.
Upasuaji
huo ulikuchukua kiasi cha saa moja unusu ambapo inaelezwa kuwa umefanyika
salama na kwa mafanikio makubwa.
Taarifa
hiyo inasema hali ya Rais Kikwete inaendelea vizuri japo bado yuko wodini
akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba.
No comments:
Post a Comment