Liberty
Stadium Usiku wa hapo jana ilikuwa ni nderemo baada ya wenye Nyumba Swansea
City kutoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuifunga Arsenal Bao 2-1 kwenye Mechi ya Ligi
Kuu England.
Arsenal walipata Bao lao Dakika ya 63 baada ya
Oxlade-Chamberlain kuunasa Mpira katikati ya Uwanja na kuwachambua Wapinzani
wawili kisha kumpasia Cazorla ambae haraka alimpelekea Danny Welbeck na
kumhadaa Beki mmoja na kumsogezea Alexis Sanchez aliefumua Shuti lililomshinda
Kipa wa zamani wa Arsenal, Lukas Fabianski.
Dakika ya 75, Swansea walisawazisha kwa Frikiki murua ya
Gylfi Sigurdsson aliyopiga kutoka Mita 25 na kumshinda Kipa Szczesny.Frikiki
hiyo ilitokana na Rafu ya Gibbs kwa Barrow.
Bao hilo lilitokana na kazi njema ya Jefferson Montero
aliempita Calum Chambers na kutumbukiza Krosi iliyopigwa Kichwa na Bafetimbi
Gomis na kutinga wavuni.
Ushindi huu umewapaisha Swansea hadi Nafasi ya 5 na
kuwashusha Arsenal Nafasi ya 6.
Ligi Kuu England sasa itakuwa nje kupisha Mechi za Kimataifa
na Arsenal watarejea Uwanjani Jumamosi Novemba 22 wakiwa kwao Emirates kucheza
na Manchester United.
Baada
ya kipigo hicho BOSI wa Arsenal Arsene ameungama kuwa Msimu huu hakuna Timu
yeyote itakayowashika Vinara wa Ligi Kuu England amabao baada ya Mechi 11
wanaongoza wakiwa kwa mbele kwa tofauti ya pengo la Pointi 4 mbele ya Timu ya
Pili Southampton. Nyuma ya Southampton wapo Mabingwa Watetezi Manchester City
ambao wako Pointi 8 nyuma ya Chelsea.
Wenger
ameeleza: “Wakiendelea hivi, inaonyesha hakuna atakaeikamata Chelsea! Kwa sasa
hakuna anaeonyesha hivyo!”
Jumamosi,
wakiwa huko Anfield, Chelsea walitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuichapa Liverpool
Bao 2-1. Ligi Kuu England sasa imesimama kupisha Mechi za Kimataifa na itarejea
tena kilingeni Jumamosi Novemba 22 na Siku hiyo Arsenal wako kwao Emirates
kucheza na Manchester United.
VIKOSI:
Swansea
City: Fabianski; Rangel, Bartley, Williams,
Taylor; Carroll, Ki; Emnes (Barrow - 67'), Sigurdsson, Montero; Bony (Gomis -
76').
Akiba: Amat, Britton, Gomis, Tiendalli, Tremmel, Fulton,
Barrow.
Arsenal: Szczesny; Chambers, Mertesacker, Monreal, Gibbs;
Flamini (Wilshere - 79'), Ramsey (Walcott - 79'); Oxlade-Chamberlain, Cazorla,
Sanchez; Welbeck.
Akiba: Rosicky, Podolski, Wilshere, Walcott, Sanogo,
Martinez, Bellerin.
RATIBA/MATOKEO:
**Saa za Bongo
Jumapili Novemba 9
Sunderland 1 Everton 1
Tottenham 1 Stoke 2
West Brom 0 Newcastle 2
Swansea 2 Arsenal 1
++++++++++++++++++++++
MSIMAMO
NA
|
TIMU
|
P
|
GD
|
PTS
|
1
|
Chelsea
|
11
|
17
|
29
|
2
|
Southampton
|
11
|
18
|
25
|
3
|
Man
City
|
11
|
10
|
21
|
4
|
West
Ham
|
11
|
5
|
18
|
5
|
Swansea
|
11
|
4
|
18
|
6
|
Arsenal
|
11
|
6
|
17
|
7
|
Man
United
|
11
|
3
|
16
|
8
|
Newcastle
|
11
|
-2
|
16
|
9
|
Stoke
|
11
|
-1
|
15
|
10
|
Everton
|
11
|
2
|
14
|
11
|
Liverpool
|
11
|
-1
|
14
|
12
|
Tottenham
|
11
|
-2
|
14
|
13
|
West
Brom
|
11
|
-2
|
13
|
14
|
Sunderland
|
11
|
-7
|
12
|
15
|
Hull
|
11
|
-2
|
11
|
16
|
Aston
Villa
|
11
|
-11
|
11
|
17
|
Crystal
Palace
|
11
|
-6
|
9
|
18
|
Leicester
|
11
|
-7
|
9
|
19
|
QPR
|
11
|
-11
|
8
|
20
|
Burnley
|
11
|
-13
|
7
|
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumamosi Novemba22
1800
Chelsea v West Brom
1800
Everton v West Ham
1800
Leicester v Sunderland
1800
Man City v Swansea
1800
Newcastle v QPR
1800
Stoke v Burnley
2030
Arsenal v Man United
Jumapili Novemba 23
1630
Crystal Palace v Liverpool
1900
Hull v Tottenham
Jumatatu Novemba 24
2300
Aston Villa v Southampton
No comments:
Post a Comment