JANA Wenyeji wa
AFCON 2015, Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, Morocco, walishindwa kuijibu
CAF kama wataruhusu Mashindano hayo kuchezwa kama ilivyopangwa kuanzia Januari
17 baada ya awali kuomba yaahirishwe kutokana na tishio la Ugonjwa wa Ebola.
Wiki
iliyopita, CAF ilikataa maombi hayo ya Morocco na iliwataka wawe wameamua
ifikapo Jana kama watakubali Mashindano hayo yachezwe kama yalivyopangwa au la.
Wiki
iliyopita, CAF ilikataa maombi hayo ya Morocco na iliwataka wawe wameamua
ifikapo Jana kama watakubali Mashindano hayo yachezwe kama yalivyopangwa au la.
Vile
vile CAF ilizitaka Nchi ambazo ziko tayari kuchukua nafasi ya Morocco
kujitokeza ifikapo Jana ili wafikiriwe kupewa Uenyeji wa Fainali hizo
zilizopangwa kuanza Januari 17 hadi Februari 8 Mwakani.
CAF
inatarajiwa kutoa uamuzi wake wa nini kifanyike kuhusu AFCON 2015 mara baada ya
Kikao chao cha Kamati Kuu ambacho kitafanyika Mjini Cairo, Misri hapo Jumanne
Novemba 11.
Licha
ya kuigomea AFCON 2015, Mwezi ujao Morocco wanatarajiwa kuwa Wenyeji wa
Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu.
Akiongelea
kuhusu sakata hili, Katibu Mkuu wa CAF, Hicham El Amrani, amesema wao hawawezi
kuruhusu Mashindano yeyote kufanyika iwapo ipo hatari yeyote na ndio maana
waliongea na Shirika la Afya Duniani, WHO [World Health Organisation], ili
kupata ushauri wao ambao ni kutoruhusu mkusanyiko wa Watu wengi kwa Nchi
zilizoathirika na Ebola tu.
Ugonjwa
wa Ebola umeshaua Watu wanaokaribia 5,000 na wengi wao ni wa Nchi za Afrika ya
Magharibi na hasa Nchi za Liberia, Guinea na Sierra Leone kwa mujibu wa WHO.
Hivi
sasa AFCON 2015 ipo hatua ya Makundi ambayo itatoa Nchi 15 kuungana na Mwenyeji
kucheza Fainali hizo na katika hizo Nchi ziliziathirika na Ebola na zenye
nafasi ya kwenda Fainali ni Nchi moja tu ambayo ni Guinea..
Lakini
cha kushangaza, Guinea, ambayo CAF ilizuia Mechi zake za Nyumbani zisichezwe
Nchini humo kutokana na Ebola iliruhusiwa na Morocco hiyo hiyo inayoogopa Ebola
kucheza Mechi zake zote za Nyumbani Mjini Casablanca Nchini Morocco.
No comments:
Post a Comment