STRAIKA wa Klabu ya
Yanga, Mrisho Ngassa, ameingia kwenye Rekodi rasmi za Afrika baada ya kuibuka
kuwa Mfungaji Bora wa CAF CHAMPIONZ LIGI Msimu wa 2014 akiwa na Bao 6
akifungana na Wachezaji wengine Watatu.
Wengine
waliofunga Bao 6 kwenye Mashindano hayo ambayo ES Setif ya Algeria iliibuka
kuwa Mabingwa ni El Hedi Belameiri wa Setif, Firmin Ndombe Mubele wa AS Vita ya
Congo DR na Haythem Jouini wa Esperance ya Tunisia.
Hii
ni mara ya kwanza kwa Mtanzania kuingia kwenye Chati aina hii kwenye Mashindano
ya Barani Afrika.
+++++++++++++++++++++++
CAF
CHAMPIONZ LIGI 2014
WAFUNGAJI
BORA:
**Wote
Bao 6
-Mrisho
Ngasa [Yanga, Tanzania]
-Haythem
Jouini [Espérance Tunis]
-Firmin
Ndombe Mubele [AS Vita, Congo
DR]
-El
Hedi Belameiri [ES Setif,
Algeria]
+++++++++++++++++++++++
Ngassa
alifunga Bao zake zote 6 dhidi ya Komorozine ya Visiwa vya Comoro waliyokutana
nayo Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONZ LIGI mapema Mwaka huu.
Kwenye
Mechi ya kwanza Jijini Dar es Salaam Ngassa alipiga Bao 3 Yanga waliposhinda
7-0 na marudiano huko Comoro, Ngassa tena alipiga Hetitriki Yanga ikishinda
5-1.
Raundi
iliyofuata Yanga walikutana na waliokuwa Mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri
na kubwagwa nje.
Ngassa,
mwenye Miaka 25, Mwaka 2009 aliwahi kwenda kufanya majaribio huko England na
Klabu ya West Ham na vile vile huko Marekani na Klabu ya Seattle Sounders Mwaka
2011 na kucheza Mechi dhidi ya Manchester United waliyofungwa 7-0.
Hapa
Nchini pia ameshazichezea Klabu za Kagera Sugar, Azam FC na Simba.
No comments:
Post a Comment