ACP KASHAI
|
KUTOKANA na matukio ya kujichukulia sheria mkononi
yanayo endelea kushika kasi mkoani Tanga Jeshi la polisi mkoani hapa limetoa
rai kwa wakazi kuachana na vitendo hivyo kwani ni kinyume cha sheria na ni kosa
la jinai.
Rai hiyo imetolewa
na kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Tanga Fressar Kashai wakati akizungumza na
waandashi wa habari katika mkutano uliofanyika ofisini jijini TANGA.
Kamanda kashai
amesema kumekuwa na matukio ya wananchi
kujichukulia sheria mkononi pasipo kujua kuwa wana vunja sheria jambo
ambalo halipo kisheria.
Kashai pia amesema
mnamo tarehe 06 Nov mwaka huu majira ya saa moja usiku huko kijiji cha Mapanga
Kata na Tarafa ya Kwekivu Wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga mwanaume mmoja alie
fahamika kwa jina la Sharifu Selemani mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa kijiji
cha Mapanga alijeruhiwa kwa kukatwa na panga mkono wa kushoto na mke wake
aitwae Gladness Daniel 18.
Hata hivyo kamanda
kashai amesema majeruhi amelazwa katika hospitali ya KKKT Songe na hali yake
inaendelea vizuri ambapo imebainika kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa
kimapenzi aliokuwa nao mtuhumiwa huyo ambae ni mke wake.
Aidha kamanda
kashai ameeleza kuwa mtuhumiwa wa tukio hilo amekamatwa na atafikishwa
mahakamani muda wowote kuanzia sasa baada ya upelezi wa awali kukamilika.
No comments:
Post a Comment