MODRIC NJE MIEZI MITATU.
SHIRIKISHO la Soka la Croatia
limethibitisha kuwa majeruhi aliyopata kiungo wa Real Madrid Luka Modric
yatamuweka nje ya uwanja mpaka Februari mwakani. Nyota huyo mwenye umri wa
miaka 29 alipata majeruhi hayo katika kipindi cha kwanza cha mchezo wa kufuzu
michuano ya Ulaya mwaka 2016 kati ya Italia na Croatia mbao ulimalizika kwa
sare ya bao 1-1. Modric alitolewa nje na kwenda kufanyiwa vipimo jijini Madrid
ambapo majibu yake yameonyesha atakaa nje kwa muda wa miezi mitatu.
Katika taarifa yake shirikisho hilo
lilidai kuwa nyota huyo hatahitaji upasuaji kwani tatizo lake litakwisha kwa
matibabu ya kawaida. Modric sasa anatarajiwa kukosa michuano ya Klabu Bingwa ya
Dunia itakayofanyika nchini Morocco mwezi ujao.
NURI SAHIN NJIANI KUREJEA UWANJANI.

Hata hivyo, Sahin mwenye umri wa
miaka 26 sasa anakaribia mwishoni kupona huku akikiri hasikii maumivu yeyote na
anahitaji kurejea uwanjani haraka iwezekanavyo. Sahin aliandika katika ukurasa
wake wa mtandao wa kijamii kuwa anatamani kurejea tena uwanjani baada ya
maumivu aliyokuwa akisikia kuondoka.KOLN
YAKANUSHA KUMTAKA PODOLSKI.

No comments:
Post a Comment